Tangazo

June 25, 2012

NAPE ANOGESHA MAHAFALI YA WANA-CCM CHUO KIKUU CHA TEKU MBEYA

Nape baada ya kuwasili mjini Mbeya kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo.

Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengerema akimkaribisha nape kuzungumza kwenye mahafali hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Tawi la CCM Chuo Kikuu cha TEKU  Boniface Paulo.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wanachama wa CCM, tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) Mbeya, katika mahafali ya kuwaaga, leo Juni 25, 2012, katika hoteli ya Paradise mjini Mbeya.

Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akimpa kadi ya CCM Aranora Msigwa wa mwaka wa  tatu, Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) alipopokea wanachama wapya wa CCM, wakati wa mahafali ya wana-CCM tawi la Chuo hicho mjini Mbeya, leo June 25. Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa  wa CCM Mbeya, Maganga Sengerema.

Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akishiriki kucheza muziki wa mtindo wa 'Kwaito' wakati wa sherehe za mahafali ya wana-CCM  tawi ala Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) katika hoteli ya Paradise mjini Mbeya leo June 25.

Wana_CCM tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) Mbeya wakimpa zawadi ya picha yake, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye wakati wa mahafali ya wana-CCM tawi la chuo hicho.

Wana-CCM tawi la TEKU wakifurahi wakati wa kwenye mahafali yao yaliyofanyika uykumbi wa hoteli ya Paradise mjini Mbeya.

No comments: