Tangazo

June 28, 2012

Pambano la Masumbwi Ubingwa wa Taifa kufanyika Julai 15

Issa Omar akinolewa na Mwalimu wake, Ibrahim Bigright
Kaike Promotion imeandaa pambano lingine la Ubingwa wa Taifa Kati ya BAINA MAZOLA na JUMA FUNDI (ambae alishawahi gombea mkanda wa dunia nchini Philipines), litakalopigwa Jumapili ya tarehe 15/07.

Pambano hili ni mtiririko wa mapambano ya ubingwa wa ngumi na kuendeleza vipaji vya mabondia chipukizi na wale tunaowategemea kwenda kuchukua mikanda mikubwa ya dunia.

Inafahamika wazi kwa taifa letu kuwa mchezo wa ngumi ni miongoni mwa mchezo unaopeperusha vema Bendera ya Tanzania lakini ni mchezo usio na wafadhili wala wadhamini unajiendesha wenyewe kwashidashida ambapo wadhamini wangejitokeza kudhamini ngumi wangelisaidia sana taifa letu.

Mchezo wa Julai 15, utasimamiwa na TPBO na mapambano yamepangwa na Ibrahim Kamwe chini ya uratibu wa Kaike Siraju yataongozwa na
mapambano ya utangulizi kati bondia anayechipukia kwa kasi Issa Omar (kutoka Bigright Boxing Mwananyamala) na Ramadhan Kumbele ambaye ni Bingwa wa Taifa kutoka Kambi ya Matumla-Keko.

Anthony Mathias (aliyekuwa bingwa wa PABA) ataminyana na chipukizi Mwaite Juma wa Bigright Boxing.

Mapambano mengine ni kama ifuatavyo hapo chini: 

DATE; 15 / 07 / 2012
VENUE; DDC Kariakoo, Dar Es Salaam, TANZANIA
PROMOTER; Kaike Promotion
MATCHMAKER; Ibrahim Kamwe
TICKETS; +255 715 707777

Bantam weight - Juma Fundi v/s Baina mazola - 10 round ,TPBO title Fly weight- Ramadhan Kumbele v/s Issa Omar - 6 round Bantam weight - Anthony Mathias v/s Mwaite Juma - 6 round super feather weight - doi miyeyusho v/s shaban mtengela 6 round light weight - Bakari mohamed v/s sadiki momba - 6 round.

No comments: