Tangazo

June 21, 2012

Wakazi zaidi ya 100,000 kunufaika na Mradi wa Uvunaji Maji ya Mvua uliofadhiliwa na SBL mjini Iringa

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akizindua rasmi mradi wa uvunaji maji ya mvua uliopo Hospitali ya Wilaya ya Iringa iliyopo Frelimo mjini hapo jana. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na kugharimu zaidi ya Shilingi Milioni 50 na unataraji kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo zaidi ya 100,000. Wengine kutoka kushoto ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu, V Mushi.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akimshukuru Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda (kulua), kwa kampuni yake kufadhili mradi huo muhimu wa maji Hospitalini hapo.

No comments: