Tangazo

July 3, 2012

MRATIBU MKAZI WA UN AWATAKA WAJASIRIAMALI KUTAFUTA SOKO LA BIDHAA ZAO NJE YA NCHI

Dkt. Alberic Kacou (kulia) akikaribishwa na Msaidizi (Ushirikishwaji Habari Umma) wa UNHCR Bw. Austin Makani alipotembelea katika banda la Umoja wa Mataifa Tanzania.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (katikati) akizungumza na Afisa Mawasiliano wa Shirika la Kazi nchini (ILO) Bw. Magnus Minja (kulia) pamoja na Bw.Austin Makani wa UNHCR alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa.

Dkt. Kacou (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mata Enterprises Company Bi. Tabby Oguma ambaye ni mmoja wa wajasiriamali wanaowezeshwa na shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu bidhaa wanazotengeneza ikiwemo jiko la kupikia (Cooking Basket).


Dkt. Alberic Kacou akitazama magauni ya Batiki yanayotengenezwa na Kampuni hiyo.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou akiweka saini kitabu cha wageni katika banda la UN Tanzania lililopo katika banda kubwa la Ali Hassan Mwinyi katika maonyesho ya 36 ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar. Kulia ni Bw. Magnus Minja wa ILO na Kushoto ni Bw. Austin Makani wa UNHCR.

Dkt. Alberic Kacou katika picha ya pamoja na wafanyakazi  shirika la Umoja wa Mataifa wanaotoa huduma katika banda la shirika hilo.

No comments: