Bw. Asah Andrew Mwambene ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika
 Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuanzia tarehe 01 Julai,
 2012. Bw. Mwambene anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Clement 
Mshana ambaye mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la 
Utangazaji Tanzania (TBC).
Bw.
 Mwambene (41) kabla ya uteuzi huu alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha 
Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa 
Kimataifa. Aidha, Bw. Mwambene amewahi kufanya kazi katika Kampuni ya 
Magazeti ya Serikali (TSN) akiwa mwakilishi wa Kampuni hiyo huko 
Zanzibar.
Idara ya Habari (MAELEZO) ndiyo Msemaji Mkuu wa Serikali hapa nchini.
IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI 
NA MICHEZO
AGOSTI 1, 2012

No comments:
Post a Comment