Trekta 64 za wakulima wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, ambazo wamezipata kwa jitihada za diwani wa kata hiyo, Omary Kariati kutoka Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT, zikiwa zimeegeshwa eneo la mkutano ulioitishwa na diwani huyo, kwa ajili ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji wa kata hiyo, hivi karibuni. Wakulima hao walifika na trekta hizo na kuwa mstari wa mbele kuchangia mradi huo wa maji. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
|
No comments:
Post a Comment