Tangazo

August 7, 2012

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL ATEMBELEA MABANDA YA MAONYESHO YA NANE NANE DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo jinsi ya uzalishaji wa zao la Zabibu kutoka kwa Ofisa Mtafiti Msaidizi wa Kilimo wa Kanda ya Kati Dodoma, Richard Malle, (wa pili kulia) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012. Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu mbegu ya mizabibu, kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mrosso (kushoto) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza.

Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisikiliza maelezo jinsi mashine za kukamulia miwa zinavyofanya kazi, kutoka kwa Mjasiliamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kiwanda cha Sukari.

Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akikagua moja ya matrekta ya kuvunia mazao aina ya Mahindi, Ngano na Mtama, wakati Makamu alipotembelea katika maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni.


No comments: