Tangazo

August 28, 2012

Mbio za Mbuzi za Hisani Dar es Salaam 2012 Zaja

Mwanzilishi wa Mbio za Mbuzi za Hisani  Dar es Salaam, Paul Joynson-Hicks (katikati) akizuingumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam laao kuhusu mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Septemba 1 mwaka huu katika Viwanja vya The Green, Barabara ya Kenyatta, jijini humo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa mbio hizo, Karen Stanley na baadhi ya wadhamini wa mbio hizo.
Dar es Salaam
MASHINDANO ya 12 ya Mbio za Mbuzi za Hisani yapo mbioni na yanatarajiwa kufanyika Septemba 1 Mwaka huu waandaaji wameeleza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mbio hizo, Karen Stanley anasema  “Mashindano yam bio za Mbuzi za mwaka huu yatakuwa ya kusisimua zaidi kuliko ilivyowahi kutokea”. Tuna mbio za mbuzi kama kawaida. Tuna aina mbalimbali za vyakula kutoka kwa watayarishaji bora wa hapa jijini wakati wa mbio hizo, michezo na burudani za watoto na michezo ya kupima uwezo wao kwa umri wowote. Hii sio ya kukosa.

Watu zaidi ya 3000 huudhuria mashindano haya kila mwaka na wengi hushiriki katika mashindano ya mavazi ya aina yake ya kuvutia yenye zawadi za kuvutia. 

Bi Stanley anaongeza; “ Mwaka huu kukiwa na kauli mbiu ya ‘Zama hizo katika nchi za Magharibi’ itawafanya watu wengi wakija huku wamevaa kama wachunga ng’ombe wa kimarekani wa zamani ‘cowboys’ wakiwa na mabuti na makofia makubwa, japo si lazima uje na muonekano huo.

Mbio za mbuzi za mwaka huu zinatarajiwa kuanza  saa 6.00 mchana hadi saa 12.00 jioni katika Viwanja vya The Green kwenye Barabara ya Kenyatta jijini Dar es Salaam..

Ukiacha mbio hizo kuwa ni kitu cha kuburudisha, lakini pia zina makusudi mengine muhimu.

Tukio hilo la kifamilia linalofanyika kila mwaka tayari limeshafanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi milioni 544 (zaidi ya dola 345,000 kwa kiwango cha sasa) kutoka kwa karibu makundi 50 ya wahisani wa ndani tangu lilipoanza mwaka 2001. (Tazama maelezo chini kwa mbio za mwaka huu.)

Asasi  mbili zitakazopewa msaada mwaka huu ni, Kidzcare Tanzania na Kigamboni. Community Centre.

Asasi  ya Kidzcare huendesha kitujo cha watoto wenye mahitaji na kituo cha watoto wadogo mjini Bagamoyo, Pwani na vituo vingine viwili Mkoani Mbeya. Kwa pamoja vikiwa na watoto wanaokaribia 300.

Asasi ya Kigamboni Community Centre hutoa elimu kwa watoto wadogo na shughuli nyingine za ubunifu wa sanaa na michezo kwa ajili ya vijana ikisaidia vijana takriban 300. Wacheza sarakasi wa asasi ya KCC watakuwa kivutio kikubwa kwa watoto watakofika katika mbio za mbuzi za mwaka huu.

Mwanzilishi wa Kidzcare,Rob Notman anasema, “Ukiangalia maisha ya mtoto mmoja utaona ni jinsi gani yamebadilika, shukrani kwa ufadhili unaotokana na fedha za Mbio za Mbuzi. Sio mabadiliko ya kimwili lakini pia maisha yote kwa ujumla, ni ajabu”.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kigamboni Community, Nassoro Mkwesso anasema,  “Watoto hapa hawana fursa nyingi, lakini wale wanaokuja hapa kituoni wanaanza kuamini kuwa wanaweza kuwa watu fulani. Baadhi wana ndoto fulani na KCC inawasaidia katika kufanya ndoto zao kuwa kweli”.

Mwanzilishi wa Mbio za Mbuzi za Dar es Salaam Paul Joynson-Hicks anasema, “Siri ya mafanikio za mbio hizi za hisani ipo katika mchanganyiko wa burudani na nia ya kutaka kuleta mabadiliko katika maisha ya watanzania. Tunachukua mitazamo yote kwa makini mno.

“Na tusingeweza kufanya hayo kwa namna yoyote bila ya wafadhili wetu, wale wanaolipa ili kumiliki mbio. Wamiliki wa mbio za mwaka huu ni Hoteli ya Southern Sun, Shirika la Ndege la British Airways, Kampuni ya Vinywaji Baridi ya  Coca-Cola, Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited, British Gas, aetna and Mantra Tanzania.”

Tiketi moja ni Shilingi 5,000 na zitauzwa getini. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti www.goatraces.com, au tuma barua pepe: goatraces@goatraces.com au piga simu 0755 555 900.

No comments: