Tangazo

August 22, 2012

Mwekezaji arekebisha mipaka yake Kinyenze, sasa wananchi kulima mashamba yao

 
LILE sakata la ardhi lililokuwa likikikabili Kitongoji cha Kinyenze, huenda sasa likafikia tamati baada ya mwekezaji wa awali kuondoka na kuja mwekezaji mpya  na kutaka suluhu na wananchi.
Mwekezaji huyo amefika kijijini hapo hii leo na kuzungumza na wananchi na kupata undani wa mgogoro huo na kuamua hapo hapo kurekebisha mipaka ya shamba hilo inayolalamikiwa na wananchi.
Akizungumza kutoka kijijini hapo mmoja wa wakazi wa Kinyenze Joseph Gomba ‘Sugu’ amesema kuwa Mzungu huyo ameagiza mipaka ifuate ramani iliyoelezwa na wananchi walime mashamba yao ambayo yalikuwa kizuizini kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Wananchi wa Kinyenze walikuwa wakilala mika juu ya Mwekezaji wa Kampuni ya TANBREED LTD  iliyonunua shamba 296 lililopo Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali, Wilayani Mvomero mkoani Morogoro, kuingilia mashamba yao na kuwazuia kufanya shughuli yeyote ya kilimo.
Ingawa juhudi za wananchi kutaka serikali ya wilaya na Mkoa kuingilia kati suala hilo iligonga mwamba kwa baadhi ya viongozi wa wilaya kuyumbisha mpango wa kukutana na mwekezaji wa awali kuzungumzia sakata hilo.
Mbunge wa jimbo la Mvomero, Amos Makala ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo amekuwa akilizungumzia sakata hilo la ardhi kijijini hapo bila mafanikia.
Baadhi ya wananchi wamefurahishwa na maamuzi ya mwekezaji huyo ambaye pia ametaka ushirikiano na wananchi hao.
“Tumefurahi sana sasa hapa hatuna kinyongo lakini vinginevyo hapa pasinge elewaka, lakini midhali kamuru njia ifunguliwe na mashamba yetu tulime sasa hatuna neono,” alisema mmoja wa wananchi.
 
 
Uzio uliokuwa umewekwa na Mwekezaji huyo wa awali ambao ulifunga njia na mashamba ya wananchi sasa utafunguliwa wakati wowote na wananchi kulima mashamba yao. 

No comments: