Tangazo

August 17, 2012

REDDS MISS ILALA 2012: Warembo 15 watakaopanda Jukwaani Sept 07 Watambulishwa

 Mratibu wa Shindano la Redds Miss Ilala 2012, Gadner G. Habash, (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge wakati wa utambulisho wa warembo 15, watakaoshiriki kwenye fainali ya Redds Miss Ilala 2012, ambapo washindi watafanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye fainali ya Redds Miss Tanzania 2012. (wa pili kulia) ni mmoja wa waratibu wa shindano hilo, Juma Mabakila, (kushoto) ni Cylivia Mashuda na (kulia) ni Neema Mbula ambao ni walimu wa warembo hao. Warembo hao watashiriki kwenye kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika Septemba 7, 2012 kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge.

Warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Redds Miss Ilala wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa  utambulisho. Picha na Intellectuals Communications Limited.

No comments: