Tangazo

September 19, 2012

WAFANYABIASHARA WA UINGIZAJI NA USAFIRISHAJI MADAWA KUTOKA CHINA NA TZ WAKUTANA DAR



Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  wa Wafanyabiashara wa Uingizaji na Usafirishaji wa  Dawa na  Vifaa tiba kutoka China, wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo wa siku moja uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Sept.19.2012. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)

Makamu wa Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Uingizaji na Usafirishaji wa Dawa na Vifaa tiba kutoka China (CCCMHPIE), Meng Dongping akizungumza  katika mkutano huo. Bi. Dongping alisema Tanzania ni nchi ya 11 katika ushirikiano wa kibiashara wa bidhaa hizo barani Afrika na nchi ya pili kwenye soko la bidhaa hizo wa nchi za EAC. ambapo katika kipindi cha miezi 6 cha mwaka 2012 ukuaji wa soko la bidhaa hizo nchini Tanzania umefikia dola za  Marekani milioni 32.61 sawa na asilimia 47.

Makamu wa Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Uingizaji na  Usafirishaji wa dawa na vifaa tiba kutoka China (CCCMHPIE) Meng Dongping (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa nchini (TDFA), Haiiti Sillo.

Mdau wa mkutano huo kutoka (MSD ) nchini, Cosmas Mwaifani akiwasilisha mada yake.

Wadau wakibadilishana mawazo.

Picha ya pamoja baada ya mkutano huo.

No comments: