Tangazo

September 3, 2012

WAJUMBE WA MKUTANO WA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA SADC WAANZA KUWASILI ZANZIBAR

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

Wajumbe wa Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SARPCCO) wameanza kuwasili mjini Zanzibar tayari kwa  kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika Septemba 5, mwaka huu.

Wajumbe waliowasili leo ni pamoja na Mkuu wa INTERPOL. Kanda ya nchi za Kusini mwa Afrika zilizopop Harare nchini Zimbabwe Bw. Chilika Simfukwe, pamoja na maafisa wengine wa ofisi hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesma mkutano huo utafunguliwa na Makam wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Gharib Bilali.

Awali Mkutano huo  ulitarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Kikwete ambaye atakuwa na shughuli nyingine za kitaifa.

Kamishna Mussa amesema kuwa wengi wa wajumbe watakaowasili mjini Zanzibar ni wale wa mikutano midogo midogo ya Kamati Tendaji za Wataalam wa vitengo mbalimbali vya Majeshi ya Polisi kutoka nchi wanachama mikutano ambayo itafanyika kuanzia Septemba 3 hadi 4, mwakahuu.

Amesema kuwa mazimio yatakayofikiwa na kila kamati, yatafikishwa na kuchambuliwa  na Wakuu wa Majeshi ya Polisi katika mkutano wao wa Septemba 5, mwaka huu.

Amesema kuwa wakati wa mkutano huo, kutafanyika gwaride maalumu la kukabidhi kitara kwa Mwenyekiti mpya wa Shirikisho hilo ambacho ni alama ya  uwenyekiti wa Shirikisho hilo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, anatarajiwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo kutoka kwa Mkuu wa Jeshio la Polisi Afrika ya Kusini kamishna Jenerali Bi. Mangwashi Phiyega anayemaliza muda wake.

No comments: