Tangazo

October 15, 2012

Kamanda Liberatus Barlow aagwa leo katika Uwanja wa Nyamagana

        Afande George Msangi akiongoza ratiba za kumuaga aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Liberatus Ballow aliyeuawa usiku wa kuamkia jumamosi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri karibu na Hotel ya Tai Five.

 Msafara wa magari ya kuleta mwili wa marehemu Liberatus Ballow yakiingia katika uwanja wa Nyamagana ili viongozi na wananchi mbalimbali wapate kuuaga mwili huo.


Maaskari walioteuliwa kubeba mwili wa marehemu Liberatus Ballow wakiwa wamejipanga vyema ili mwili uweze kutolewa ndani ya gari ili uwekwe sehemu nzuri ambayo kila mtu anaweza kuuaga vizuri.

        Hapa wakiushusha kutoka ndani ya gari ili waweze kuubeba.

 Safari ya kuelekea sehemu maalum iliyopangwa kwa ajili ya mwili wa marehemu ilianza hivi.

Viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakisimama kwa dakika chache kuupa heshima mwili wa marehemu kamanda Liberatus Ballow.

        Baadhi ya Maafisa ya Jeshi la Polisi waliofika uwanjani hapo.



        Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Ballow.

         Maafisa wa Polisi wakitoa saluti kwa Marehemu Kamanda wa Mkoa wa Mwanza Liberatus Ballow wakitoa heshima za mwisho.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga akiweka saini katika daftari la maombolezo katika msiba wa marehemu kamanda Liberatus Ballow katika uwanja wa Nyamagana.


Wanafamilia wa marehemu wakiwa na majonzi makubwa sana katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa mpendwa wao Liberatus Ballow.Picha kwa Hisani ya B Plus Blog


No comments: