Tangazo

October 23, 2012

TBL YASAIDIA MILIONI 40.5/- MRADI WA UCHIMBAJI VISIMA HANDENI

 Mkuu wa Wilaya ya Handeni,akipokea mfano wa hundi ya sh 40.5 milioni  kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo  kwa ajili yakuendeshea mradi wa uchimbaji wa visima 15 vya maji katika vijiji vitano vya Kata ya Kwangwe,Wilaya ya Handeni,Mkoa wa Tanga, mradi huo unaotazamiwa kukamilika mara baada ya miezi mitatu.

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto) akimkabidhi Diwani wa Kata ya Kwamgwe, wilayani Handeni, Tanga, Shariffa Abebe mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 40.5  akipokea hundiya sh 40.5 zilizotolewa na kampuni ya TBL kwa ajili ya kuchimba visima 15 katika vijiji vitatu vya kata ya Kwamgwe.

 Diwani wa kata ya Kwamgwe Wilaya ya Handeni,Shariffa Abebe akiishukuru Kampuni ya TBL kwa  kutoa kiasi cha sh 40.5 milioni kwa ajili ya kuchimba visima 15 vya maji katika vijiji vitatu vya Kata ya Kwamgwe.

Diwani wa Kata ya Kwamgwe,Wilaya ya Handeni,Mkoa wa Tanga,Shariffa Abebe akipitia ratiba ya hafla ya uzinduzi wa mradi wa uchimbaji wa visima 15 katika vijiji vitatu vya kata hiyo vilivyofadhiliwa na kampuni ya TBL iliyotoa kiasi cha sh 40.5 milioni. Mradi huo ulizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Muhingo Rwenyemamu aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Chiku Gallawa.

No comments: