Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (waliokaa mbele wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu utaratibu wa usajili wa magari ya Umma na kuwepo kwa zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote. Serikali imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba za kiraia yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma .
Baada ya hapo Operesheni kamata kamata magari, pikipiki, Bajaj na mitambo ya umma, itaanza na vilevle kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT, JW, DFP, CW, SM na SU.
Kwa mujibu wa Dk. Magufuli, hadi sasa serikali imeshasajili vyombo vya moto, 123,431 yakiwemo magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma. Mkuu wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga. PICHA/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO
|
No comments:
Post a Comment