Tangazo

January 16, 2013

AFRICAN BARRICK GOLD (ABG) BULYANHULU GOLD MINE 'FAMILY DAY' YAFANA

Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu na familia zao wakichangia damu zoezi lililoendeshwa wakati wa  Siku ya Wanafamilia wa Mgodi huo katika viwanja vya Gofu mgodini hapo Wilayani Kahama hivi karibuni. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Wakati wa maakuli uliwadia... Ni misosi kwa kwenda mbele ushindwe wewe tu.



Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) Bulyanhulu, Dennis Hoof akifungua rasmi sherehe hizo za Siku ya Wanafamilia. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya AKO Catering Services na Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylvester Koka na Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, Bi. Isabela Chilumba.



B Band wakitumbuiza katika sherehe hizo.

Rock Drill Competition

Maonyesho ya Uokoaji.


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) Bulyanhulu, Dennis Hoof (kushoto), akikabidhi zawadi ya 500,000/- kwa Wilson Dominician Kazinja baada ya kuibuka mshindi wa pili katika shindano la upasuaji miamba 'Rock Drill Competition'.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) Bulyanhulu, Dennis Hoof (kushoto), akikabidhi zawadi ya 700,000/- kwa Abdul Urasa baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la upasuaji miamba 'Rock Drill Competition' lililofanyika wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia wa Mgodini hapo Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Bodi ya AKO Catering Services Ltd na Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylvester Koka akibadhi kikombe kwa mshindi wa jumla wa shindano la table tennis, Prakash Uthirapathy (kulia).  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa AKO Catering Services Ltd, Ponziano Mponzi, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) Bulyanhulu, Dennis Hoof na (kushoto) kwa Mh. Koka  ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, Bi. Isabela Chilumba.

Usiku ulipowadia mambo ya masebene ya kukata na shoka yaliporomoshwa na B Band.


BABA NA MWANA: Kiongozi wa B Band, Banana Zorro (kushoto), na baba yake mzazi Mzee Zahir Ally Zorro wakifanya mavituziiii....

Kundi zima la B Banda wakilishambulia jukwaa.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) Bulyanhulu, Dennis Hoof (katikati) akishow love na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo.

Mratibu wa Mawasiliano wa Mgodi huo, Bi. Reji akienda sambamba na Banana Zorro.

Meneja Mkuu wa Bulyanhulu Gold Mine Ltd, Dennis Hoof  akicheza na mmoja wa wafanyakazi ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo kwa wafanyakazi wake.

Mambo ya mduara, Lucy yuleeeeeeeeeeeeeeeeeee.......akitabasamu.

No comments: