Tangazo

January 15, 2013

IGP AKABIDHI PIKIPIKI KWA WAKAGUZI WA TARAFA NCHINI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema (kulia), akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova kama ishara ya kukabidhiwa Makamanda wote Tanzania Bara na Visiwani ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania Bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini dar. PICHA/ HASSAN MDEME WA JESHI LA POLISI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kikosi cha Mbwa na Farasi Tanzania Mrakibu wa Polisi Eugen Emmanuel, kwa ajili ya matumizi ya Programu ya Usalama wetu Kwanza.jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza.PICHA/ HASSAN MDEME WA JESHI LA POLISI

Baadhi ya Wakaguzi wa Tarafa wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wakiwa katika pikipiki zao baada ya kukabidhiwa katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza.PICHA/FRANK GEOFRAY WA JESHI LA POLISI

No comments: