Tangazo

February 12, 2013

HOYCE TEMU AIFARIJI FAMILIA YA DAUDI MWANGOSI NA KUIPA MKONO WA KHERI




Hoyce Temu akimpa mkono wa pole mke wa Marehemu Daudi Mwangosi alipoitembelea familia hiyo kuifariji.
Mwanaharakati wa kijamii Hoyce Temu kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania amefanya ziara mkoani Iringa na kupitia nyumbani kwa familia ya mwandishi aliyeuawa Daudi Mwangosi na kuwajulia hali.
Hoyce Temu kwa pamoja na kundi zima la waandaaji wa kipindi cha mimi ni Tanzania waliwasili katika nyumba ya mjane huyo Bi. Itika Mwangosi kumsabahi na kutaka kujua anaendeleaje na maisha kila siku.
Hoyce Temu akimfariji mke wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi alipoitembelea familia hiyo mkoani Iringa.
Ziara hiyo nyumbani hapo ni kwa nia nzuri ya kutaka kujua jinsi anavyokabiliana na changamoto za kila siku za maisha pamoja na watoto wake wanne.
Walizungumza mengi yakiwemo yale yanayomkwaza Bi. Itika Mwangosi na jitihada anazofanya ili kujikwamua.
Aidha Bi. Temu akiwa amewapakata watoto wa marehemu aliifariji familia hiyo akiwataka kutokata tamaa na kuwa Mungu yupo na kwa kuwa watanzania ni wamoja mambo yatakwenda sawa.
Hoyce Temu akiwapa kumbatio la upendo watoto wa marehemu Daudi Mwangosi.
Bi. Itika Mwangosi akionyesha uso wa matumaini baada ya kupewa maeneo ya faraja na Hoyce Temu.
Amezungumza na watoto kuhusu kwenda shule na kutaka kujua wanasoma shule gani na iko umbali gani kutoka nyumbani.
Pamoja na mambo mengine Hoyce Temu kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania amewasihi watanzania wenye moyo wa ukarimu kumsaidia Mjane huyo ambaye hana ajira kwa hivyo ni vigumu kupata kipato cha kujitosheleza yeye na wanawe kwa mahitaji muhimu ya kila siku.
Watoto wa Marehemu wakionyesha matumaini mapya baada ya kufarijiwa na Hoyce Temu.
Mtanzania mwenye ufariji kwa familia hiyo anaweza kutuma kiasi chochote cha fedha kwenye namba inayomilikiwa na mjane huyo Mama Itika Mwangosi kupitia mtandao wa M-Pesa: 0767670739 ili msaada huo uwafikie walengwa.

No comments: