Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi hii ya Februari 16, 2015 amekwenda kuhani na kufariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani iliyotokea Februari 11, 2013 na kupoteza maisha ya watu tisa papohapo wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli la mizigo.
Familia alizokwenda kuhani na kuzifariji ni pamoja na za marehemu Hassan Erasto Kurunge (57), Maria Sadiki ((52) na mtoto wa mwaka mmoja Samweli Ismail wa kata ya Ubena.
Wengie ni marehemu Essau Enos Mwamgingo (16) , Stella Isaack Kazimoto (18), Bahati George Mbena (17) na Latifa Maneno (17)
Akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Ahmed Kipozi, Rais Kikwete alieleza kusikitishwa kwake kwa ajali hiyo, na kuwataka madereva wawe makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani
Rais Kikwete alisikitishwa zaidi kwa taarifa kwamba gari hilo dogo lilikuwa limebeba abiria wanane, na kuwa dereva wake ambaye pia alipoteza maisha, hakuwa makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani.
No comments:
Post a Comment