Watafiti na
wanasayansi nchini Tanzania wametakiwa kufanya tafiti za kiungunduzi ambazo
zitaleta manufaa na kusaidia jamaii ya watanzania .
Hayo yamesema
na leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele
Malecela(pichani juu) wakati
wa semina ya siku moja ya wagunduzi mbalimbali iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya
NIMR na Shirika la Grand Challenges la nchini Canada.
Dkt.
Malecela amesema umefika wakati sasa kwa wagunduzi mbalimbali wa Kitanzania
kuanza kungundua njia mbalimbali za kuweza kutatua matatizo yaliyopo katika
jamii hasa katika sekta ya afya.
Semina
hiyo ya siku moja ilikuwa na lengo la kuhamasisha wangunduzi sekta ya afya
ambapo baadhi ya wanasayansi wagunduzi kadhaa walitoa taarifa zao za awali za
namna ya kukabiliana na matizo kadha hasa kwa Mama na mtoto.
Wagunduzi
kadhaa waliweza kuzungumzia gunduzi zao katika semina hiyo na miongini mwa hizo
ni pamoja na ile ya hali ya Utapiamlo unaofanywa na Dkt. Magreth Kagashe kutoka
Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Bianadamu Ifakara ambayo inafanyika katika
Vijiji vya Kilombero.
Ugunduzi
mwingine ni wa namna ya kusafisha maji na kuyaweka katika hali salama kupitia
njia ya Takasa maji, na kuyaweka taika hali salama nay a usafiugunduzi unaofanya
na Kijakazi Mashoto na Ugunduzi mwingine ni matumizi ya Maua ya Rosella katika
kukabiliana na Upungufu wa damu kwa mama na mtoto.
Dkt.
Malecela amesema ya kuwa ugunduzi unaofanyika sasa na kupewa fedha na Grand
Challenge ya Canada unatakiwa uwe ugunduzi ambao utaleta mabadiliko na kubadili
maisha ya wananchi.
“Mara
nyingi wanasayansi wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali na kugundua matatizo
mengi katika jamii lakini mara chache watafiti hawa wametafuta suluhisho ya
hayo matatizo au magonjwa katika jamii hizo ...kwahiyo hivi sasa wanasayansi wagunduzi
wa kitanzania umefikia hatua ya kugundua vitu ambavyo vitasaidia jamii,” alisema
Dkt.Malecela.
Aidha
nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer alisema kuwa
jumlya ya miradi 16 ya ugunduzi inayofanywa na wanasayansi wa kitanzania
itapatiwa fedha kupitia taasisi hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya semina hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya NIMR jijini Dar
es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela
akipiga picha na Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand
Challenge Canada, Peter Singer mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Makao
Makuu ya NIMR jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment