Tangazo

April 10, 2013

Dhifa ya kumpongeza Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya Kuapishwa

Rais Jakaya  Kikwete akimpongeza Rais Mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta huko Ikulu mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa nne wa nchi hyo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa kimataifa wa michezo wa Moi-Kasarani jijini Nairobi tarehe 9.4.2013.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais aliyemaliza muda wake Mheshimiwa Mwai Kibaki huko ikulu jijini Nairobi mara tu baada ya sherehe ya kumwapisha Rais Mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru  Kenyatta kumalizika huko uwanja wa Moi Kasarani tarehe 9.4.2019

Marais Jacob Zuma wa Afrika Kusini (kushoto), Rais Jakaya Kikwete na  Bongo wa Gabon wakifanya mazungumzo kwenye ikulu ya Nairobi mara baada ya kumalizika sherehe ya kuwaapisha viongozi wakuu wa Kenya zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Moi Kasarani tarehe 9.4.2013.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na wake wa viongozi wa juu wa Kenya, Mama Magrate Kenyatta (kushoto) ambaye ni mke wa Rais Uhuru na Mama Recheal  Ruto (kulia) Mke wa Naibu Rais wa nchi hiyo Mheshimiwa William Ruto huko ikulu jijini Nairobi mara tu baada ya kuapishwa  viongozi hao tarehe 9.4.2013.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria dhifa ya kitaifa Mama Salma Kikwete, Rais aliyemaliza muda wake Mwai Kibaki, Rais Mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta , Rais Jakaya Kikwete na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margarate Kenyatta wakisikiliza wimbo wa Taifa la Kenya ukipigwa kabla ya kuanza dhifa hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya ikulu jijini Nairobi tarehe 9.4.2013.

Rais Jakaya Kikwete kwa niaba ya viongozi wengine waliohudhuria sherehe za kuapishwa viongozi wapya  akimshukuru Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wa  Kenya kwa kufanikisha uchaguzi na sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa nchi hiyo.

Rais Mpya wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta akiwashukuru Marais na wakuu wa nchi waliohudhuria sherehe za kumwapisha wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa huko ikulu jijini Nairobi.

Baadhi ya Marais na wakuu wa nchi wakiwa na wake zao katika picha ya pamoja huko ikuku jijini Nairobi baada ya kumalizika sherehe ya kumwapisha rasmi Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto.

No comments: