Tangazo

April 10, 2013

Maafisa Mawasiliano wa Taasisi mbalimbali za Serikali wajifunza kutumia mitandao ya kijamii

Hivi karibuni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uingereza nchini  imewapatia mafunzo ya  kuwajengea uwezo Maafisa  Mawasiliano kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali jinsi  ya kutumia mitandao ya kijamii katika kuimarisha mawasiliano. Mafunzo hayo yameendeshwa na  Taasisi ya Thomson Foundation na kugharamiwa na Serikali ya Uingereza. Pichani  Mkufunzi wa Mafunzo David Wiggins (katikati) akifurahia zawadi ya shati la kitenge baada ya kukabidhiwa na Afisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi  Judith Mhina (kushoto ) kwaniaba ya wenzake, (kulia) ni Mkurugenzi  wa Idara ya Habari Assah Mwambene.

Maafisa Mawasiliano Serikalini wakiwa katika picha ya pamoja. baada ya kumaliza  mafunzo ya  jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii  kama facebook,twitter, flickr nablogs.

Mkufunzi kutoka  Uiengereza David Wiggins akiwaaga Maafisa Mawasiliano Serikalini (hawapo pichani) baada ya kumaliza  mafunzo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) .PICHA/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO

No comments: