Tangazo

April 16, 2013

Mstahiki Meya Jerry Silaa abariki Bonanza la Stakishari Veterans FC kutimiza Miaka Mitano


Picha juu na chini ni Mgeni rasmi Mh. Mstahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza wananchi pamoja na washiriki wakati wa bonanza la timu ya Stakishari Veterans FC kutimiza miaka 5 ambapo amesema mpira wa soka unawakutanisha watu na kuwasidia kujenga mahusiano pamoja na kujenga afya za miili yao.
Picha juu na chini Mgeni rasmi Mh. Mstahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi jezi na mipira kwa baadhi ya timu 17 zilizoshiriki katika bonanza hilo.
Diwani wa Kata ya Kipawa Mheshimiwa Bonna Kaluwa akigawa jezi na mipira kwa timu zilizoshiriki Bonanza la Stakishari Veterans kutimiza miaka 5.
Mgeni rasmi Mh. Mstahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akijiandaa kupiga penati kuashiria ufunguzi wa Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Stakishari kata ya Gongo la Mboto jijini Dar.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akionyesha ufundi na kufunga goli wakati akipiga penati ya kuzindua rasmi bonanza la Stakishari Veterans FC kutimiza miaka 5.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipongezwa na Golikipa aliyemfunga goli kwa penati wakati akizundua Bonanza hilo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu ya Stakishari Veterans FC iliyofanya Bonanza la kutimiza miaka 5 Kipawa jijini Dar.
Bonanza likirindima katika viwanja vyaStakishari Kipawa kata ya Gongo la Mboto baada ya kupewa baraka na Mstahiki Meya Jerry Silaa.

Timu zilizoalikwa kushiriki Bonanza la Sitakishari VSC

New Ukonga Veteran - Ukonga, Pugu Kajiungeni Veteran - Pugu, Pugu Kigogo Fresh Veteran -Pugu, Segerea Veteran - Tabata, Kivule Veteran - Kivule, Kipunguni B Veteran - Kipunguni, Kinyerezi Veteran - kinyerezi, Tabata Veteran - Tabata, Bandari Veteran - Kurasini, Mbagala Veteran - Mbagala, Makangarawe Veteran - Mbagala, Airport Veteran - Airport, Kisukulu Veteran – Kisukulu Tabata, Kigamboni Veteran - Kigamboni, Vingunguti veteran - Vingunguti, na Wenyeji Sitakishari veteran.

No comments: