Tangazo

April 16, 2013

NIMR YAANZA MKUTANO WAKE 27 WA WANASAYANSI WATAFITI JIJINI ARUSHA LEO

 
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) leo imeanza mkutano wake wa 27 wa mwaka kwa watafiti Wanasayansi jijini Arusha ambapo Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein anataraji kuufungua rasmi jioni ya leo.

Pamoja na Mkutano huo wa NIMR, pia mkutano wa pili wa Wanasayansi kuhusiana na Masuala ya Afya barani Afrika unafanyika sambamba na mkutano huo ambapo watafiti mbalimbali duniani wanatoa mada juu ya tafiti mbalimbali za magonjwa ya binadamu.

Mkutano huo ambao umebeba kauli Mbiu ya Mabadiliko ya Mazingira katika Utafiti wa Afya 'Changing landscape in Health Research' utafanyika kwa siku nne katika Hotel ya Snow Crest jijini Arusha.


Pichani ni Dk. Jeff Waage kutoka Uingereza akiwasilisha mada juu ya Kilimo na Afya katika Mabadiliko ya Mazigira katika Utafiti wa Afya.

Baadhi ya washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Arusha hii leo. Baadhi ya Wabunge nao wamealikwa kushiriki katika mkutano huo.

No comments: