Tangazo

May 25, 2013

African Barrick Gold (ABG) yatoa Madawati 2,360 yenye thamani Milioni 480/- kwa Shule za Msingi Wilaya ya Kahama

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Anselm Tarimo ( kulia), akikata utepe kama ishara ya kupokea madawati 2,360 yenye thamani ya 480m / - kwa shule 15 za msingi za serikali katika wilaya ya Kahama yaliyotolewa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) kupitia migodi yake ya Buzwagi Gold Mine na Bulyanhulu Gold Mine kwa uratibu na Hassan Maajar Trust (HMT) katika hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi ya Mwendakulima wilayani Kahama jana. Wengine (kutoka kushoto) ni Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa ABG, Stephen Kisakye, Mwakilishishi wa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Dennis Sebugwao na Makamu Mwenyekiti wa HMT, Shariff Maajar. PICHA/JOHN BADI

African Barrick Gold (ABG) kupitia mfuko wake wa ABG Maendeleo Fund imetenga Shilingi Bilioni 1.6 kwa ajili ya ununuzi wa madawati kwa shule za Mikoa ya Kanda ya Ziwa.


   Msanii wa ngoma za asili kutoka katika kijiji cha Mwendakulima akitumbuiza wakati wa hafla hiyo.

Meza kuu.

Maofisa Waandamizi wa ABG wakifutalia kwa makini tukio hilo. Kutoka (kushoto), Bw. Swai kutoka Buzwagi Gold Mine, Blandina Munghezi kutoka ABG Dar es Salaam na Salome Makamba kutoka Buzwagi.

Makamu Mwenyekiti wa Hassan Maajar Trust, Shariff Maajar akihutubia katika hafla hiyo.


Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa Buzwagi Gold Mine, Dennis Sebugwao akitoa hotuba yake.

Wasanii wa ngoma za asili kutoka katika kijiji cha Mwendakulima akitumbuiza wakati wa hafla hiyo.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwendakulima wakiwa wamekalia sehemu ya madawati yaliyotolewa msaada na ABG.

RAS wa Shinyanga, Dk. Anselm Tarimo akihutubia wakati wa hafla hiyo.

Maofisa Waandamizi wa ABG wakifuatilia kwa makini hafla hiyo.Kutoka (kushoto), Mose kutoka Buzwagi Gold Mine na Sara kutoka ABG Dar es salaam.

Picha za pamoja zilipigwa baada ya hafla hiyo.




No comments: