Tangazo

May 10, 2013

Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka Afrika Mashariki wakutana na Wanahabari jijini Dar

Mwenyekiti wa  Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka wa Afrika Mashariki, Dk. Eliezer Feleshi akitoa ufafanuzi wa jambo katika mkutano wa waandishi wa habari  uliofanyika jijini Dar es Salaam Mei 10,2013  kwaajili ya kutoa maazimio ya mkutano wa siku mbili uliowakutanisha  Wakurugenzi  wa Mashtaka wa Afrika  Mashariki. Nchi zinazojumuisha shirikisho hilo ni kutokaTanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.  PICHA/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO

Rais wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka wa  nchi za Afrika Mashariki Martin Ngoga (kushoto) akitoa taarifa ya  maazimio ya mkutano wao wa siku 2  kwa waandishi wahabari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salam. Kutoka (kulia) Mkurugenzi wa Mashtaka wa Uganda , Richard Buteera,  Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka Afrika Mashariki, Dk. Eliezer Feleshi , akifuatiwa na  Mwendesha Mashtaka kutoka  Burundi , Valentine Bugorikunda.

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia  hotuba ya Rais wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka wa Afrika Mashariki.

Mwandishi wa habari wa magazeti ya TSN , Abdul Saliboko akiuliza swali.

No comments: