Tangazo

July 24, 2013

Airtel, UNESCO wazindua Mradi wa kuwezesha Radio za Kijamii nchini

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe akisalimiana na baadhi ya watoto wa mtandao wa wanahabari alipowasili kwenye uzinduzi wa kurusha matangazo ya Redio FADECO kwenye mnara wa Airtel wilayani Karagwe mkoani Kagera, kulia kwake ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe akijianda kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi huo, anayeshuhudia tukio hilo ni  Meneja Mahusiano ya Jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi na wa kwanza kulia ni Meneja wa Biashara wa Kanda wa Airtel Ally Maswanya.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe akitoka kukagua mnara wa Airtel uliounganishwa Redio ya Kijamii ya FADECO. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Redio ya kijamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO Joseph Sekiku (katikati) wakati hafla ya uzinduzi huo. Kushoto ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi.

Meneja wa Kituo cha redio ya Jamii FADECO, Adelina Lwedamula (kushoto), akitoa maelezo machache ya utengenezaji wa vipindi kwa Meneja Mahusiano ya Jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi alipotembelea Studio za Redio hiyo inayorusha matangazo yake kwenye mnara wa Airtel ambapo itawezesha kupanua wigo wa matangazo yao kwa jamii.
**********************************
 .Zaidi ya watu milioni mbili sasa kufikiwa na mawasiliano ya Radio FADECO kufuatia uzinduzi huo.

Airtel Tanzania kwa kushirikiana na lisilo la kiserikali la United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO) wamezindua mradi wa kuwawezesha radio za kijamii kwa kuwapatia vifaa vya radio na kuwaunganisha na mitambo ya mawasiliano ili kuwafikia wananchi wa pembezoni
kwa urahisi zaidi.

Airtel na UNESCO) kupitia mradi huo watawawezesha wananchi wa pembezoni kupata taarifa na matangazo mbalimbali ya kijamii, kiutamanduni , Kiuchumi na kupata elimu juu ya maswala mbalimbali ya kijamii.

Mradi huo wa kipekee ulizinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Masawe ambae aliwatia moyo Airtel na UNESCO kuendelea na moyo huo wa kusaidia jamii kupitia radio zao za kijamii ambazo ndio zipo karibu na wananchi wa vijijini. Aidha aliwataka wananchi wa Karagwe kuitumia radio hii kwa maendeleo ya jamii na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika uzinduzi rasmi wa mradi katika radio ya FADECO Karagwe, Meneja Mahusiano ya Kijamii, Hawa Bayumi alisema kwamba mradi huo kwa kushirikiana na UNESCO utawanufaisha watu wa pembezoni ambao radio za kijammii (Community Radios) ndio kimbilio lao la karibu katika kupata habari na taarifa mbalimbali.

Alisema radio za kijamii ni radio za kipekee ambazo zinawafikia kwa urahisi watu wa pembezoni katika kupata taarifa za elimu ya jamii, Afya, uchumi, ujasirimali na stadi za maisha ili kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi. Radio za kijamii zina uwezo wa kuwafikia wananchi kwa haraka zaidi na radio hizo zipo karibu na wananchi aliongeza Bayumi

 “kwa upande wake Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Aminalisema tupo na ushirikiano na radio za jamii kama nane na leo tumeanza na radio ya Fadeco . maendo mengine yatakayonufaika na mradi huu ni pamoja na Sengerema Mwanza,  Chake Chake Pemba, Makunduchi Unguja , Pangani Tanga, Kyela Mbeya , Kahama Shinyanga, Loliondo Arusha  na Uvinza Kigoma.

Al Amin alisema radio za jamii ni muhimu katika kuelimisha wakinamama na maswala ya ujasirimali, uzazi wa mpango na ni wadau muhimu katika kuleta maendeleo kwenye jamii husika. radio za kijamii ni mdau mkubwa wa kuwawezesha na kuwafundisha wananchi umuhimu wa kufanya kazi ili kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa radio FADECO bwana Joseph Sekiku alisema tunawashukuru sana Airtel na UNESCO kwa kuboresha ufanisi wa huduma zetu za radio hapa Karagwe , sasa radio yetu inaweza kusikika kwa usikivu zaidi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya karagwe na wilaya za  jirani kama vile Wilaya ya Kyirwa, Wilaya Missenyi, wilaya ya Bukoba vijijini na mjini, wilaya ya Muleba,  Biharamuro  na Ngara , hii ni takribani watu wapatao zaidi ya milioni 2 sasa wanapata mawasiliano ya radio tofauti na ilivyokuwa awali. Kwa kweli haya ni mafanikio makubwa na tunawashukuru sana kwa hilo.

Kupitia mradi huo kampuni ya Airtel imeweza kuwapatia modem na simcard radio za kijamii ili kuwawezesha waandishi wao wa Habari kufanya kazi kwa ufanisi.

Mradi wa Radio ni program maalum inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na UNESCO yenye lengo la kusaidia jamii zilizo na changamoto mbalimbali ikiwemo za mila potofu, elimu duni, ukeketwaji, imani za kishirikina, maendeleo duni , ukandamizaji wa wanawake na watoto na changamoto nyingi zinginezo. Lengo hasa ni kuinua mawasiliano katika maeneo ya vijiini nchini.

No comments: