Tangazo

July 24, 2013

MASELE AWAPA RUNGU TMAA, AWAAGIZA KUWAKAMATA WANAOTOROSHA MADINI

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akizungumza katika Baraza la Wafanyakazi wa TMAA leo jijini Dar es Salaam.

NA MWANDIHI WETU
SERIKALI imeiagiza Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), kuwakamata wanaotorosha madini.

Pia, imeiagiza TMAA kuhakikisha inaokoa rasilimali za nchi ili ziweze kulinufaisha taifa na wananchi wake na umeutaka wakala huo, kuwabana wachimbaji wadogo ili walipe kodi stahiki za serikali.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifungua mkutano wa tatu wa baraza la wafanyakazi la TMAA.
Alisema Wakala huo, uhakikishe kuwa serikali inapata mapato stahiki kutoka kwenye shughuli za uzalishaji na biashara za madini.

Masele alisema katika kufanikisha hilo, TMAA isiache kuwakamata wale watakaobainika wanatorosha madini nje ya nchi.

"Naomba muwakamate watakaobainika wanatorosha madini yetu, mukifanya hivyo mutakuwa mumetekeleza wajibu wenu," alisema.

Alisema jukumu lingine ambalo TMAA inapaswa kulipa kipaumbe ni kuhakikisha inaokoa rasilimali za nchi.

Masele alisema miongoni mwa rasilimali za nchi ni pamoja na madini hivyo amewataka wakala huo kuhakikisha inaisimamia vya kutosha rasilimali hiyo.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, TMAA iongeze juhudi za kukusanya mapato ikiwa ni pamoja na kuwabana wachimbaji wadogo ili walipe kodi.

Alisema kiasi kikubwa cha fedha kinapotea kutokana na wachimbaji wadogo kukwepa kulipa kodi.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TMAA, Mhandisi Paulo Masanja, alisema wakala huo umepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake.

Alisema moja ya mafanikio hayo ni kwamba baadhi ya wamiliki wa migodi mikubwa nchini kuanza kulipa kodi ya mapato ambapo, kuanzia 2009 hadi sasa wamekusanya sh. bilioni 473.9.

Mhandisi Masanja alisema kutokana na ukaguzi wa kimkakati uliofanywa na wakala huo , sh. bilioni 1.8 na wachimbaji madini ya ujenzi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kama mrahaba.

Alisema baraza la wafanyakazi la wakala huo, liliundwa kwa mujibu wa sheria na lilianzishwa Mai 5, 2011.

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Paulo Masanja akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala huo, lililoketi jijini Dar es Salaam, jana. Anayefuata ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele.
WAJUMBE wa Baraza la wafanyakazi la WAkala wa Madini Tanzania (TMAA) wakiwa kwenye kikao cha baraza hilo kilichofanyika jana Dr es Salaam.
WAJUMBE wa Baraza la wafanyakazi la WAkala wa Madini Tanzania (TMAA) wakiwa kwenye kikao cha baraza hilo kilichofanyika jana Dr es Salaam.
MJUMBE wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Madini Tanzania (TMAA), akitoa mada kwenye mkutano wa baraza hilo uliofanyika jana mjini Dar es Salaam.
  WAJUMBE wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Madini Tanzania (TMAA) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Masele baada ya kufungua kikao cha Baraza.
 WAJUMBE wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Madini Tanzania (TMAA) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Masele baada ya kufungua kikao cha Baraza. Imetayarishwa na theNkoromo Blog

No comments: