Tangazo

July 5, 2013

Mkutano wa Wajumbe wa Baraza la Katiba la Tasnia ya Habari Kanda ya Dar es Salaam wafanyika jijini Dar leo

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Katiba la Tasnia ya Habari Kanda ya Dar es salaam, ulioundwa na MCT lililofanyika Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo. Wajumbe wa baraza hilo walikutana kuichambua na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuboresha Rasimu ya Katiba ya Mpya ya Tanzania wakijikita zaidi katika masuala ya Haki ya Kupata Habari, Uhuru wa Vyombo vya Habari na Haki ya Kujieleza. Wa (pili kushoto), ni Mwenyekiti wa mkutano huo, Allan Lawa na (kulia) ni Meneja Udhibiti na Viwango wa MCT, Bi. Pili Mtambalike. PICHA/JOHN BADI 


 Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa katika mkutano. PICHA/JOHN BADI 

  Sehemu ya Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa katika mkutano. PICHA/JOHN BADI 
 
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Tasnia ya Habari anayekiwakilisha Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT), John Badi akichangia maoni yake wakati wa mkutano huo. Wengine ni Baraka karashani anayewakilisha Tanzania press Centre (wa pi kulia) na Aloyce Ndeleio anayewakilisha kampuni ya Media Solutions Ltd. PICHA/RICHARD MWAIKENDA

No comments: