Tangazo

July 8, 2013

Umoja wa Mataifa yanyakua Tuzo Maalum katika Maonyesho ya 37 ya Biasharaya Kimataifa jijini Dar

photo (26)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yaliyofikia tamati jana kwenye viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar. Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou.
photo (29)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ( wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Wajasiriamali wanaofadhiliwa na UNIDO kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa akiwa ameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda (kushoto) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou (wa pili kulia) wakati wa sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa jijini kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
photo (33)
Tuzo maalum waliyokabidhiwa shirika la Umoja wa Mataifa nchini kwa kutambua mchango wao wa kuhamasisha Jamii (UN Special recognition for community awareness) wakati wa sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
photo (25)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dk. Alberic Kacou akipokea Tuzo ya Ngozi iliyotengenezwa kinyumbani kutoka kwa Wajasiriamali wanaodhaminiwa na UNIDO wakati alipotembelea Banda la Shirika hilo leo kwenye maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara yalifungwa rasmi jana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
photo (31)
Mkufunzu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) Marwa Wambura (kulia) akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou ya malighafi za ngozi zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali na wajasiamali wanaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza viwanda Duniani (UNIDO).
photo (24)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini. (UN-Tanzania Delivering as one).
photo (30)
Banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba likiwa limeandika ujumbe unaosema "Umoja wa Mataifa inafanya kazi kwa ajili yako-kuboresha maisha ya watoto, wakinamama na vijana".
photo (28)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakiwa ni wadau washirika wa Maendeleo nchini.
photo (27)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na mmoja wa wadau alipotembelea banda la Wizara ya Fedha ikiwa ni kudumisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania.

No comments: