Mkurugenzi
Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti wakwanza kushoto akifatiwa na mwakilishi
wa Be Forward bw Kohei Shibata na Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson
Mmbando kwa pamoja wakimkabithi Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP
Mohamed Mpinga stika za usalama barabarani kwa mwaka huu. Airtel, Puma pamoja
na Be Forward ni wadhamini wa wiki ya usalama barabarani kwa mwaka huu.
*******************************
Dar
es salaam 19, Septemba 2013
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya mafuta PUMA na
Be Forward kwa pamoja wameungana na baraza la taifa la usalama barabarani
na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kuhakikisha elimu
kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti idadi ya ajali za barabarani
nchini.
Kutangazwa kwa ushirikiano huo kumefanyika leo
katika makao makuu ya Usalama Barabarani jijini Dar Es Salaam ambapo Naibu Kamishna wa Polisi
(DCP) Mohamed Mpinga ametangaza wiki ya nenda kwa usalama barabarani ya mwaka
huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Mwanza.
Akiongea wakati wa halfa hiyo mkuu wa Naibu
Kamishna wa Polisi DCP Mohamed Mpinga alisema” nachukua fursa hii kuwashukuru
wadhamini wa kampeni ya usalama barabarani kwa mwaka huu kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel, Kampuni ya Mafuta ya PUMA na kampuni ya magari Be Forward
kwa kutoa mchango wao wa pamoja na kushirikiana na jeshi
la polisi usalama barabarani kufikia malengo kwa kuhakikisha usalama wa raia na
kupunguza ajali za barabarani.
Ajali za barabarani zinaongezeka kwa kasi na
kusababisha upotezaji wa nguvu kazi huku zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni
jukumu la kila mtanzania kuwa sehemu ya kusimamia na kuzingatia sheria za
barabarini huku tukiishi na kutimiza kauli mbiu ya mwaka huu “Usalama
Barabarani unaanza na mimi
wewe na sisi sote”.
Nachukua fursa hii kuwaaasa watumiaji wa vyombo
vya moto kupeleka magari yao
kukaguliwa na kuthibitishwa ubora wa kutembea barabarani ili kuhakikisha vyombo
vinavyotumika kubeba abiria viko salama na vinakidhi viwango vilivyowekwa
kuhakikisha usalama barabarani.” aliongeza Mpinga
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkuu wa kitengo
cha mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema “kwa muda wa miaka mitano sasa
Airtel tunajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya watanzania
na mali zao na tunayo dhamira ya kuhakikisha tunashirikiana na wadau wote wenye
wito wa kusaidia
usalama barabarani na jeshi la polisi
usalama barabarani kupunguza ajali za barabarini kwani moja ya dhamira ya
Airtel ni moja kati ya shughuli za kijamii tunazozifanya nchini.
Nia na madhumuni yetu makubwa ni kusaidia
shughuli zinazofanywa na jeshi la polisi kusimamia na kupunguza matokeo ya
ajali za barabarani, kila mwaka kunakua na matukio ya ajali za barabarani
ambazo zingeweza kuepukika kama wahusika
wangekua na elimu ya kutosha. Hii ndio sababu kubwa na madhumini ya Airtel kuwa mmoja wa washiriki wakuu katika
kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha upungufu wa ajali
barabarani kwa muda wa miaka mitano sasa.”.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya mafuta ya
PUMA ENERGY Mkurugenzi Mkuu wa PUMA ENERGY ndugu Philippe Corsaletti alisema
“Sisi kama Puma Energy Tanzania
tunaamini katika kufanya shughuli zetu za kibiashara katika mazingira ambayo ni
salama na yasiyokua na madhara kwa jamii iliyotuzunguka na pasipo kuharibu
mazingira. Wajibu huu sio kwa hapa Tanzania peke yake bali ni kila
mahali tunapokuwepo duniani.
Suala la kushirikiana na vyombo vya serikali kama Polisi kitengo cha
usalama barabarani limekuwepo kwa muda mrefu na bado litaendelea
kufanyika tena kwa nguvu na kwa upana zaidi. Katika kuitika mwito wetu wa
kuendelea kutoa mchango wetu katika kufanikisha kampeni nzima ya Usalama
barabarani, kampuni ya Puma mwaka huu imegharimia vitu mbali kama
stiker za ukaguzi, T-shirt na vitabu vya elimu vya usalama barabarani vyote
hivi vikiwa vinathamani ya shilingi za Kitanzania milioni 50.
Bado tunazidi kusisitiza kuwa ajali zote
zinazuilika na kinachotakiwa ni kila mtu kwa nafasi yake kufanya maamuzi sahihi
na kuchukua hatua zinazopaswa.
Nae Mkurugenzi mkuu wa Be Forward bw.* *Daniel
Mtaalam alisema.”tunatoa wito kwa watu wote kushirikiana nasi kufanikisha zoezi
hili na nimatumaini yetu msaada huu tunaotoa itasaidia katika kupunguza na
kudhibiti ajali zinazotokEa barabarini nakusababisha maafa makubwa kwa taifa na
jamii kwa ujumla.
Airtel Tanzania kwa mwaka huu imechangia
kuchapisha stika, kutoa elimu kwa kwa waendesha Boda Boda , mashindano ya
mpira kuhamasisha vijana pamoja na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt
500 zenye ujumbe wa mwaka huu “Usalama Barabarani unaanza na mimi wewe na
sisi sote”. Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja
atafanya sehemu yake.
No comments:
Post a Comment