Tangazo

September 20, 2013

NSSF YAIPIGA JEKI ROCKY CITY MARATHON 2013


Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini BMT, Dioniz Malinzi akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mbio za Rocky Marathon.  
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa mbio za Rocky City Marathon uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo NSSF imedhamini mbio hizo kwa kutoa sh.milioni 15. 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleima Nyambui.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Rocky Marathon 2013 Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, akizindua rasmi mbio za Rocky City Marathon 2013 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu ambao wamedhamini mbio hizo kwa kutoa sh.milioni 15. 
 Baadhi ya wadau.
Picha ya pamoja.

DAR ES SALAAM, Tanzania

MSIMU wa tano wa mbio za Rock City Marathon umezinduliwa, ambapo mdhamini mkuu Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetaka kuwepo kwa mgawanyo wa majukumu kwa mbio za umbali tofauti ili kuharakisha uendelezaji wa vipaji vya wanariadha nchini.

Rock City Marathon zinaratibiwa na Kampuni ya Capital Plus International (CPI), ambapo Ofisa Uhusiano wa NSSF inayodhamini mbio hizo kwa mwaka wa nne sasa, Juma Kintu aliliomba Shirikisho la Riadha Tanzania RT kugawana majukumu na wadau.

“Sisi kama NSSF tuko tayari kudhamini na kuchangia maendeleo ya riadha nchini, ndio maana tunasisitiza mgao wa majukumu kwa wakimbiaji wa umbali fulani kusimamiwa na taasisi au kampuni moja, ili kusaidia maendeleo ya haraka na makuzi sahihi ya vipaji,” alisema Kintu.

Pamoja na NSSF, wadhamini wengine wa Rock City Marathon 2013 zitakazofanyika jijini Mwanza Oktoba 27 ni pamoja na PPF, Airtel, African Barrick, Nyanza Bottlers, Sahara Media, Precission Air, Bank M, New Mwanza Hotel na Umoja.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, aliyekuwa mgeni rasmi, alisema mchezo wa riadha nchini unaelekea kuangamia na jitihada za kuunusuru zinahitajika.

“Ni aibu kuwa mchezo wa riadha nchini unaelekea kufa wakati viongozi waliopewa mamlaka ya kuhakikisha unaendelea wanashuhudia. Ni wakati wa kuamka kuunusuru mchezo huu ambao katika miaka ya 1970 mpaka 1980 uliiletea nchi yetu heshima kubwa.

Kwa upande wake, Rais wa RT, Suleiman Nyambui aliwataka waratibu wa marathon kote chini kuhakikisha wanakuwa na mbio fupi za vijana ili kupanua wigo wa kuzalisha vipaji vipya, vitakavyoliletea sifa taifa na kushinda mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Naye Mgurugenzi Mtendaji wa Capital Plus, Ellen Otaru Okoedion, aliishukuru Serikali kwa ahadi ya ushirikiano, lakini akaitaka kuhakikisha inakaa mezani na (kina Nyambui) RT, ili kujadili njia sahihi zitakazofanikisha kupatikana kwa kina ‘Nyambui wapya.’

Aidha, Mratibu wa tukio hilo, Mathew Kasonta alisema kuwa mbio hizo zitajumuisha  kilometa tano kwa wakimbiaji kutoka katika makampuni, kilometa tatu kwa wenye ulemavu, kilometa tatu kwa watu wazima (zaidi ya miaka 55) na kilometa mbili kwa watoto wenye umri kati ya miaka 7 mpaka 10.

No comments: