Tangazo

October 11, 2013

AIRTEL YATOSHA BABA LAO YATANUA KIFUA ZAIDI

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Bw. Levi Nyakundi akitangaza rasmi kuboreshwa kwa huduma ya Airtel Yatosha Baba lao baada ya kuongeza dakika zaidi, MB za intaneti zaidi na SMS bila kikomo kwa bei ile ile ya 999 kwa siku wakati wa hafla fupi maalum iliyofanyika leo makao makuu ya Airtel Dar es salaam.
• Kwa beil ile ile ya shilingi 999 unapata  SMS bila kikomo,  dakika 55 na MB 500 kuperuzi mitandao upendavyo.

Airtel Tanzania kupitia vifurushi vyake vya Yatosha imeendelea kujiimarisha zaidi ikiwa ni siku chache tangu kumalizika kwa promosheni yake kabambe ya shinda nyumba 3.

Akiongea kuhusiana na BABA LAO ilivyozidi kufunguka kwa kuboreshwa zaidi Mkurugenzi wa Masoko  wa Airtel Tanzania, Levi Nyakundi  alisema “Airtel Yatosha baba lao imenogeshwa zaidi tena! Tunasema yaani Ni Airtel yatosha ni Baba lao na bado itaendelea kubakia hivyo, kwa sasa kwa shilingi 999 tu mteja atapa SMS bila kikomo kwenda mtandao wowote, MB 500 za kuperuzi intanet na pia atapata dakika 55 zakupiga simu kwenda mtandao wowote nchini.

Ikumbukwe kuwa vifurushi vyote vya siku vya yatosha vinadumu kwa masaa 25 tangu mteja anapojiunga hii ni kwa lengo maalum kabisa kumfanya mteja wetu yeyote aweze kufurahia thamani ya pesa yake katika huduma zetu.

 Lengo letu ni kuona Huduma yetu ya Airtel yatosha baba lao inaendelea kuwafaidisha watanzania kuendelea kuokoa pesa nyingi zaidi walizokuwa wakitumia kwenye mawasiliano na kuanza kuzitumia katika shughuli nyingine za uchumi wa taifa na jamii kwa ujumla Kujiunga na kifurushi chochote cha SIKU, WIKI au MWEZI piga *149*99#.

Naye meneja Masoko wa Airtel Bi, Anethy Muga alisema “Ikiwa utajiunga na vifurushi hivi vilivyoongezewa muda na dakika ni hakika kabisa kuwa utaokoa pesa nyingi na utaweza kujiweka katika nafasi nzuri sana yakupanga mambo mengi ya kiuchumi kwa kuwa unaokoa pesa nyingi”.

Airtel yatosha inaendelea na mkakati wa kutosha zaidi kumtimizia mtanzania haki yake ya mawasiliano kwa kumpa mawasiliano nafuu huku Airtel pia ikihakikisha mawasiliano madhubuti yanapatikana alieleza Bi, Muga.

Promosheni ya Airtel yatosha sjhinda nyumba 3 ilikwisha mwanzoni mwa wiki hii, laikini bado huduma ya yatosha inaendea na sasa vifurushi vya huduma hiyo vimeongewa zaidi kwa lengo la kuifanya huduma hiyo kuwanufaisha wateja zaidi.

No comments: