Rais Dk. Jakaya Kikwete |
Na Anna Nkinda – Maelezo
Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa
leo jijini Dar es Salaam na kusainiwa na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wanawake
na Maendeleo (WAMA) ambayo ndiyo inamiliki shule hiyo Daudi Nasib inasema jumla ya wanafunzi wa kike 67
wanatarajia kuhitimu elimu yao
ya kidato cha nne Novemba mwaka huu.
Taarifa hiyo inasema shule ya Sekondari ya
WAMA-Nakayama ni matokeo ya
ushirikiano mzuri kati ya Taasisi ya WAMA na wadau mbalimbali wa
maendeleo kutoka ndani na
nje ya nchi wenye mapenzi ya kusaidia jamii. Bodi ya Wakurugenzi ya WAMA
iliamua Shule hiyo iitwe jina hilo
kwa heshima ya Bwana Hayao Nakayama kutoka
Japani aliyetoa msaada uliosaidia ujenzi wa awamu ya kwanza ya shule.
“Moja ya malengo ya Taasisi ya WAMA ni kusaidia upatikanaji wa Elimu
bora ya Sekondari kwa watoto wa kike na watoto wengine waishio katika mazingira
hatarishi na yatima. Na ni kwa mantiki hii ndiyo maana shule ya WAMA- Nakayama
imejengwa ili kutimiza
lengo hili.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,Mama Salma Kikwete na
Bodi ya Wakurugenzi ya WAMA
inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wadau wote wanaosaidia Shule ya WAMA-
Nakayama na kuunga mkono juhudi za Taasisi yetu”, ilisema taarifa ya Nasib.
Shule ya Sekondari ya WAMA- Nakayama ilianza mwaka 2010
ina wanafunzi wa kike 325
kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ambao ni yatima na wengine
wanatoka familia maskini, watoto hawa wasingeweza
kupata elimu ya sekondari bila ya msaada
wa Taasisi ya WAMA ambayo
huwapatia mahitaji yao yote bure ikiwemo; malazi, chakula, sare za shule,
shajara, vitabu na nauli za kwenda makwao kipindi cha likizo.
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ni Taasisi
isiyo ya kiserikali na isiyo
ya kibiashara iliyoanzishwa na Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, mwaka 2006 ina
malengo ya kuboresha maisha
ya wanawake na wasichana katika masuala
ya afya, elimu na uchumi pamoja na kutengeneza fursa za maendeleo ya wakina
mama na watoto.
No comments:
Post a Comment