Mwandishi Wetu
FOMU za mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama
Uhuru Marathon, zinatarajiwa kuanza kuuzwa rasmi kuan zia kesho, huku Rais
Jakaya Kikwete akitarajiwa kuchukua fomu namba moja.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck (pichani)
alisema, Rais Kikwete ndiye atakayepewa fomu nambo moja kwa ajili ya
kushirikishi mbio hizo.
“Hizi mbio zina maana kubwa mno ndani ya
Taifa letu, Rais Jakaya Kikwete muda wote anasisitiza na kupigania amani. Amani
ni yetu sote, si vyema kumuachia Rais Kikwete peke yake kuipigania, hivyo yeye
ndiye atakayekuwa namba moja katika kuchukua fomu na kushiriki mbio hizo,”
alisema.
Melleck alisema, katika kuhakikisha kila mtu
anashiriki kutakuwa na vituo 13 vitakavyofunguliwa kwa ajili ya kutoa fomu
hizo, huku pia kukiwa na watu maalumu watakaozisambaza maofisini na hata
majumbani.
Melleck alisema, fomu hizo zitatolewa kwa
Sh 100,000 kwa wale watakaotaka kukimbia mbio za kilomita tatu, Sh 2,000 mbio
za kilomita tano, Sh 6,000 kwa atakayeshiriki moja kati yam bio za kilomita 21
au 42.
“Hizi mbio ni muhimu zaidi kwa
ajili ya Taifa letu, hivyo ni vyema kwa Watanzania wote wakashiriki ili
kuipigania amani iliyopo nchini mwetu.
“Tunataka kuungana na Rais
Kikwete katika kuhakikisha tunakuwa sehemu ya kuleta umoja, amani na mshikamano
ndani ya Tanzania na ndilo lengu la mbio hizi.
“Bado tunaendelea kuwaomba
wadhamini wajitokeze kuzidhamini, kwani nafasi bado ipo wazi na watambue hata
wao ni sehemu ya kupigania amani ya taifa letu,” alisema Melleck.
Katika mbio hizo,
zitakazowashirikisha watu wa kada mbalimbali, zitakuwepo pia mbio za kilomita
3, kilomita 5, Half Marathon kilomita 21 pamoja na Full Marathon yenyewe
kilomita 42.
Mratibu huyo anasema mbio za
kilomita 3 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi wa kada mbalimbali, wakiwemo
pia wale wa dini na zile za kilomita 5 pia zitakuwa za kuchangia kwa ajili ya
watu wa mahitaji ya aina mbalimbali.
“Hapa tunachotaka kufanya
katika mbio za kilomita 3 ni kuwaomba kama vile viongozi maarufu wa dini
mbalimbali pamoja na viongozi wetu ili kushiriki, kwa kudumisha amani na
upendo.
“Pia tutahakikisha kama mbio za
kilomita 5, zinakuwa kwa ajili ya kuchangia watu wenye mahitaji mbalimbali na
tayari tuna uhakika mkubwa wa wanariadha maarufu zaidi duniani kushiriki,”
Alisema.
Melleck alisema, wamejipanga mno ili
kuhakikisha wanafanya mambo makubwa zaidi na ambayo yataleta tija kwa taifa.
No comments:
Post a Comment