Tangazo

September 10, 2011

MFUASI WA CCM AMWAGIWA TINDIKALI IGUNGA



Mfuasi wa CCM, Mussa Tesha (24) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, leo. Tesha ameungua usoni na sehemu kadhaa mwilini baada ya kumwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo na watu wanaodaiwa kuwa ni wafausi wa CHADEMA, ambapo inaelezwa kuwa walimwagia tindikali hiyo alipokuwa katika harakati za kubandika mitaani mabango ya mgombea wa Ubunge jimbo lgunga kwa tiketi ya CCM. Tesha alitarajiwa kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo kwa gharama za CCM. Anayemtazama ni Daktari wa hospitali hiyo, Selemani Masinga. (Na Mpigapicha Wetu)

1 comment:

Anonymous said...

Ndugu zangu waTZnafikiri tunaanza kuchanganyikiwa ukweli inaleta maana gani tunaposema tunataka demokrasia huyu ni binadamu kama wewe sioni sababu ya kumwadhibu namna hiyo pia fikirini wewe na yeye ni wafuasi tu wale ambao ni viongozi wako wa juu siajabu hawakujui wewe hebu geuza shillingi upande wa pili uwe wewe umemwagia hiyo tindikali ungejisikiaje ACHENI UJINGA NA MAMBO YA KUIGA HAYANA FAIDA TUNATAKA MAENDELEO SIO UADUI