NA
MAGRETH KINABO - MAELEZO
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante
Ole Gabriel (pichani), amewataka wasanii nchini kutumia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa ajili ya kukopa fedha za
kuendeleza kazi zao .
Profesa
Gabriel alisema hayo jana wakati
alipokutana na baadhi viongozi wa mashikisho ya wasanii na wasanii kwa nyakati tofauti
jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa
wizara hiyo.
Alisema
Serikali imetenga fedha kiasi cha Sh.
bilioni 6.1 kupitia mfuko huo, ambapo kati ya fedha hizo Sh. bilioni 1.4 za makundi
maalum wakiwemo wasanii. Hivyo ni vyema
wasanii vijana wakaanza kutumia
fursa hiyo.
Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka wasanii kuzingatia maadili na kujenga heshima
katika utendaji wa kazi zao michango ya
iendelea kutambulika kwenye jamii.
Profesa Gabriel aliyasema hayo
jana wakati alipokuwa akifunga warsha ya
siku moja kuhusu Haki miliki kwa wasanii
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Namanga jijini Dares Salaam.
Alitoa
wito kwa wasanii hao kuacha kusema
kwani tabia hiyo inaharibu majina yao kwa kuwa itakuwa ni vigumu jamii
kuthamini michango yao iwapo
watajihusisha na vitendo viovu, huku akisisitza kwamba wasanii ambao majina yao yameshajengeka katika jamii watambue kuwa huo ni mtaji wao
wasiupoteze.
Aliwataka kuanza kufanya kazi zao kibiashara
na kuwa taaluma ya biashara ili waweze kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi,
ikiwemo kutumia mapato ya kazi zao katika kufanya shughuli zingine.
Alisema
Serikali itaendelea kushirikiana na wasanii katika kukabiliana na
changamoto mbalimbali wanazozikabili.
Kwa upande wake msanii maarufu John Kitime akizungumza kwa niaba ya wenzake
alivitaka vyombo vya habari viwe vinalipia
kazi zao wasanii pale wanapotumia nyimbo zao.
Naye
mmoja wa kiongozi, Rais Shirikisho la
Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF), Simon Mwakifamba aliomba wapewe nguvu ya
kisheria ili kuweza kudhibiti maadili ya wasanii kauli ambayo ilingwa mkono na
baadhi ya viongozi wenzake.
Kwa upande wao wasanii hao , waliiomba Serikali kutawasaidia
kutatua tatizo la uharamia wa kazi za wasanii,ambapo Suzan Lewis alishauri kuwa ikiwezekana utumika mfuko
unatumika kwenye vocha za simu ambazo mtu hawezi kughushi.
Pia walipendekeza
kuwepo kwa bei elekezi ili kudhibiti
uuzaji holela kwa kazi zao.
No comments:
Post a Comment