Balozi
Hilda Komba wa shina namba 9 Tawi la Amani Makolo akimkaribisha
nyumbani kwake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa shina namba 9,katika tawi la Amani Makolo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha
Aman Makolo waliojitokeza nyumbani kwa Balozi Hilda Komba wa shina namba
9 ,Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Wanachama
wapya wa Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga wakila Kiapo cha
Uanachama wa CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
ambaye leo amefanya ziara katika wilaya ya Mbinga.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa Shina namba 9
Tawi la Amani Makolo ambapo aliwapongeza kwa ushirikiano na mshikamano
waliokuwa nao kiasi wameweza kuwa na wanachama hai 426.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kijiji
cha Mtundawalo wakati akiwasili kijijini hapo tayari kwa kufanya mkutano
wa hadhara.Katika Mkutano wa hadhara Katibu Mkuu wa CCM alizungumzia
mipango mbali mbali ya kutatua matatizo ya wananchi na kuwaeleza
wananchi CCM haiwezi kurubuniwa kwa sababu ya kupata kura,akasisitiza
wananchi wawe wa kweli kwa serikali ili haki itendeke kwa haraka.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na viongozi wengine
wa CCM kulima shamba la wanawake na vijana wajasiriamali Mkwaya kata ya
Kilimani.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajasiriamali wa
Mkwaya kata ya Kilimani ambao kwa pamoja wameamua kujishughulisha na
kilimo.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakulima wa kata ya Mkwaya .
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya Mganda wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wilayani Mbinga.
Katibu wa NEC Itikadi na uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo Mbinga mjni.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya
kukabidhi pikipiki 50 zilizotolewa na mbunge kwenda kwa watendaji wa
vijijini.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimueleza Katibu wa NEC Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose uzoefu wake wa kuendesha
pikipiki,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Ndugu Senyi Ngaga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mbinga
mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanika kwenye viwanja vya michezo
vya Mbinga mjini ambapo aliwaeleza wananchi kuwa chama cha Mapinduzi
kitasaidia kutoa ushauri kwa mazao ambayo bei yake inashuka na kupanda.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya wa zamani Ndugu Osmund Kapinga.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana
na Mzee Osmund Kapinga Mkuu wa Wilaya mstaafu mara baada ya kukamilika
mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya michezo vya Mbinga mjini mkoa wa
Ruvuma.
No comments:
Post a Comment