Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala(DACICO)Vedasto Malima, akisimamia mitihani. |
Mwalimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala (DACICO), Kasilima Kasi akiwa katika kusimamia Moja ya Chumba cha Mitihani. |
Na Mwandishi wetu
Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala Dar es Salaam City College(DACICO), kimeendelea na Zoezi la Mitihani kwa wanafunzi walioingia katika Mwezi wa Kwanza, mwezi wa sita na wale wa mwezi wa tisa ambao ni Intake January, Intake Julai na Intake Septemba katika ngazi ya Cheti na Diploma kwa ajili ya kumaliza Mafunzo yao katika Chuo kwa Uangalizi wa Mkurugenzi wa Mafunzo Dacico, Vedasto Malima.
Kati ya wanafunzi hao wanaoshiriki mitihani hiyo wapo wale wanaomaliza masomo yao na wanaotarajia kwenda kwenye mafunzo ya majaribio(Field) ambao ni wale wa intake Septemba ambao wamesoma kwa kipindi cha miaka mitatu katika ngazi ya Stashahada ya Uandishi wa Habari, na wanafunzi wa intake january ambao wamemaliza muhula wa pili nao wakiwa nanaelekea kwenye mafunzo ya majaribio (Field) kwa kipindi cha mwezi mmoja na wale wa intake julai wao wanatarajia kwa na likizo ya mwezi mmoja.
Wanafunzi hao walianza mitihani tangu jumatatu wiki hii ambapo ratiba ya masomo inaanza mapema kila siku kuanzia mbili na Nusu hadi saa tisa jioni kwa ngazi zote za Masomo ikiwa ni pamoja na wale wanaoingia masomo ya jioni, kutokana na kuwa ni waajiliwa wa maeneo mbalimbali ya sehemu walizojiajili ama kuajiliwa.
Aidha wanafunzi walioko katika mchakato wa kufanya mitihani ni tawi la Dar es Salaam, ambao wapo Kibamba CCM jijini Dar es Salaam, ambapo katika mitihani hiyo wanafunzi wameielezea kwa mitazamo tofauti kwani wapo waliosema kuwa mitihani ni migumu na wapo waliosema ni yakawaida ikiwa ni kutokana na jinsi kila mwanafunzi alivyoweza kuelewa pindi wakiwa Darasani kwa ajili ya kujifunza.
" Mitihani ni ya kawaida sana, maana walimu kwa upande wangu naona wameleta mitihani ambayo wametufundisha na kama kuna mwanafunzi anasema kuwa mitihani ni migumu basi huyo hakuwa makini darasani au inawezekana alikuwa ni mvivu wa kuhudhulia wakati wa ufundishwaji, isipokuwa sijafahamu kuhusu mitihani ya Vitendo(Practical) lakini pia nahisi itakuwa ya kawaida kwani tumejifunza kwa muda mrefu sana vifaa vyote vya mafunzo ya vitendo ikiwemo Camera za Television, Camera za Stil, Tape Recoder, na pia Utangazaji kwani kumbuka hapa chuo kuna kila aina ya vitendea kazi, zaidi ni hii Studio ya Utangazaji ya chuo ambayo inatarajia kuwa hewani muda mfupi ujao, kwani ni studio yenye kila aina ya vifaa vya kisasa, kwa hiyo nahisi tuko sawa ndugu mwandishi" alisema Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu katika Masomo ya Uandishi wa Habari na Utangazaji Deogratius Peter
Akizungumzia Mitihani hiyo Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo ha Dacico, Vedasto Malima alisema kuwa wanashukuru kuona zoezi la mitihani likienda vizuri kutokana na wanafunzi wengi kufika kwa wakati ukilinganisha na miaka ya nyumba ambapo madarasa yalikuwa machache.
" kwanza kabisa nikupongeze ndugu yetu mwandishi kwa kukumbuka kutufikia katika chuo chetu na kutaka habari ya mitihani yetu, ila kubwa ni kwamba mitihani inaendelea vizuri na wanafunzi wote wameitikiwa mwito na wanajitaidi kufika kwa wakati. kingine ni jinsi ambavyo mitihani ya mwaka huu imekuwa na hamasha hapa chuo maana kila mwanafunzi amekuwa makinin katika kuzingatia kufuata taratibu zote ususani katika kipindi hiki cha mitihani, pia namshukuru mkurugenzi wentu kwa kufanikisha kuongezab madarasa hapa chuoni kama unavyoona majengo yetu, wanafunzi wanafanya mitihani kwa furaha kutokana na kutumia madarasa makubwa yenye hewa nzuri tofauti na miaka ya nyuma, labda nichukue nafasi hii kuwataka wanafunzi wanaomaliza elimu za sekondari kuja kujiunga na chuo chetu ambacho kina matawi matatu mpaka sasa, katika mkoa wa Mbeya, Dar es Salaam na kule Sumbawanga, muda bado upo kwa wanafunzi wanaotaka kuja kujiunga kwa kipindi hiki cha intake Novemba" alisema Mkurugenzi wa Mafunzo Dacico Bwana Malima.
Wakati huo Mkurugenzi wa Dar es Salaam City College(DACICO) Bwana Idrisa Mziray alisema kuwa wamekamilisha taratibu za kupandisha Bendera ya Chuo yenye Alama na nembo za chuo pamoja na ile ya Taifa yaani bendera ya Tanzania, kutokana na kukamilika kwa majengo ya makao makuu ya chuo yaliyopo kibamba jijini Dar es Salaam.
Mziray alisema kuwa ni heshima ya pekee kwa chuo kupandisha Bendera ya chuo na ya Taifa kutokana na kwamba sasa chuo kinatambulika sehemu mbalimbali za nchi pamoja na nchi za nje na kwamba zoezi hilo la kupandisha Bendera litafanywa na kama kumbukumbu pia ya kumwapisha Rais mpya wa Serikali ya Wanafunzi Dacico pamoja na kumuaga Rais Mstaafu katika Serikali ya Wanafunzi ya Chuo cha Dacico, baada ya kufanyika mchakato wa kuwapata viongozi wa chuo katika Uchaguzi uliomalizika mwishoni mwa juma lililopita na Mathias Huleb kuibuka mshindi katika nafasi ya Makamu huku nafasi ya Urais ikichukuliwa na Mathias Canal.
"Bado tunaendelea na mapambano ya kufikia Malengo ya Chuo hadi kufikia mwaka 2015, kwani katika mpango mkakati ni kuhakikisha kwamba DACICO inapanuka na kuwa na matawi mengi hapa nchini, na pengine nikuhakikishie tu kwamba kwa sasa Dacico inajiandaa na zoezi la kuwa na kituo cha Radio(DACICO FM) na hii itakamilika punde maana tupo kwenye harakati za kukamilisha taratibu kupitia ngazi husika ambao ni mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), jambo kubwa ilikuwa ni uhaba wa madarasa ambalo sasa limemalizika ikiwa ni baada ya kuongeza madarasa kama unavyoona mwenyewe, na baada ya kupata Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi iliyokuwa ikiumiza vichwa vya wanafunzi, jukumu ni wao kula kiapo cha kuwatumikia wanafunzi wenzao kama walivyowaahidi, na nimepanga kwamba zoezi la kuwaapisha liandane na jukumu la kupandisha bendera ya Chuo pamoja na hii ya Taifa" alisema Mziray
Mpaka sasa Dar es Salaam City College kinazidi kupanuka na tayari kimepata mafanikio makubwa kutokana na kuwa na wanafunzi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, na kimekuwa ni mwanga kwa wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho kutokana na kuwapa wanafunzi taaluma ya mbalimbali ikiwemo hii ya Uandishi wa habari na Utangazaji.
No comments:
Post a Comment