Meneja wa Shamba la zao la zabibu lililopo Chinangali, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Ronaldaka akisoma taarifa ya shamba hilo, Washiriki wa semina ya Wenyeviti wa CCM kutoka kata za wilaya ya Kinondoni, mjini Dar es Salaam, walipotembelea shamba hilo, jana kujua zao za zabibu linavyozalishwa, changamoto na faida za kilimo cha zao hilo.
Meneja wa shamba akiwaonyesha mfumo wa maji unavyofanya kazi kuyavuta kutoka visimani kabla ya kumwagiliwa shambani. Wasita kushoto ni kiongozi wa msafara huo, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Mzee Madenge
Wajumbe wakionyeshana kitu wakati wakitazama bwawa maalum la maji ya kumwagilia mashamba ya zabibu
Meneja huyo akiwaonyesha wajumbe maji yanavyoingia kwenye vishina vya miti ya zabibu
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba Hassan Dalali (watatu kushoto) ambaye ni mjumbe wa semina hiyo, akiwaeleza jambo wenzake kwenye shamba la zabibu
Meneja wa shamba akimpa maelezo mkuu wa msafara mzee Madenge. Kulia aliyevaa kijani ni Katibu wa CCM, wilaya ya Dodoma mjini Saad Kusilawe. Wenyeviti wa CCM katika kata 31 za wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wapo mkoani Dodoma kwenye semina au mafunzo ya siku nne kwa ajili ya kujinoa zaidi weledi wao katika masuala mbalimbali ya kijamii na uongozi. Imetayarishwa na theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment