Na Magreth Kinabo
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)
Jaji Mstaafu Damian Libuva ametoa ufafanuzi kuwa tume hiyo iko
huru na si kweli kwamba haiko huru kama inavyonukuliwa katika
baadhi ya taarifa
na watu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Lubuva wakati
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC
jijini Dares Salaam, alisema tume hiyo iliundwa kwa mujibu wa sheria
kupitia Iba
Jaji Libuva alisema kwa muda mrefu katika
chaguzi mbalimbali yamekuwepo mlalamiko dhidi ya tume kuwa si huru
na moja ya sababu zinazotolewa ni kutokana na mfumo wa uteuzi wa
makamishina wa tume kuchaguliwa na Rais, ambaye ni kiongozi wa Chama
tawala.
“ Hili linapigiwa kelele hasa na vyama vya siasa na wadau
wengine wa uchaguzi. Mara kadhaa katika mijadala limerudiwa rudiwa na hata
baadhi ya vyombo vya habari vimenukuliwa vikisema hata Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi amekiri kuwa tume siyo huru.
Tume inafanya kazi zake za kusimamamia na kuongoza shughuli
za uchaguzi kwa uhuru ,na wazi bila kuingiliwa na chombo chochote iwe ni
seriklai au Chama
chochote cha siasa,” alisema Jaji Lubuva.
Aliongeza kuwa tume hiyo haijawahi kuagizwa kuendesha
uchaguzi kwa kupendelea chama au mgombea yeyote.
Aidha alisema katika mihadahra ambayo tume hiyo
ilialikwa msimamo wa umekuwa ukitolewa ni Tume Huru. “ Nimetoa mada
katika vyuo vikuu Iringa na Dares Salaam ambapo uhuru wa Tume umehojiwa katika
mada hizo nimesisitiza juu ya suala hilo,” alisisitiza .
Jaji
Lubuva alifafanua kuwa kwa vile mfumo uliopo wa tume hiyo ni wa Kikatiba, kama
wananchi na wadau kwa ujumla wanataka mfumo wa uteuzi wa wajumbe wa tume
ubadilike , basi wachukue fursa hiyo kutoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba
No comments:
Post a Comment