TAMKO
LA KIKAO CHA MKOA – CHADEMA
PAMOJA
NA BAADHI YA VIONGOZI WA MAJIMBO NA HII NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
- Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma 5/12/2013
-
Ambapo
atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya miwili kwa
kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano ufanyike makao Makuu ya
Jimbo. Lengo likiwa kuangalia uhai wa chama.
-
Mambo
makuu na muhimu yalizingatiwa
-
Usalama
kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe.Zitto na
mapokeo ya wanachama wetu.
-
Kutoa
taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo
yao.
-
Baada
ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa
ifuatavyo
i.
Mkoa
uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa
wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uwezekwenda katika majimbo
hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu ya kuheshimu na kuwa na
nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu yetu. Hata kama yanamaumivu
….katiba yetu ifuatwe katika kutatua tatizo – Maoni ya Wengi Mkoani
na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya k/kuu ambayo dhahiri yalilenga
kumilika Zitto – Kisiasa.
ii.
Mkoa
ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa
majimbo ya mkoa kwa hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa kiongozi wetu Dr. Slaa
kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na wapenzi wakitafakari na kwa
kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.
iii.
Kwa
hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6 kuwa hali
ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara yake kupisha
mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake Kitaifa.
iv.
Hivyo
Mkoa kupitia kikao hicho kuwa ni bora kuzuia kuliko kutibu, tayari sintofahamu
zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana mitazamo ni HATARI katika
hali hiyo. Mkoa ulijiridhisha usalama hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi
ya majimbo yakisema wao wapo salama tu.
v.
HOFU/TAHADHARI
- Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.
Mkoa hautokwepa lawama na Uzembe wa
makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu.
Hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo
hadi hali itulie na mkoa upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi
wake na hasa wa Taifa.
LENGO KUU: NI KUHAKIKISHA CHADEMA
TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA
Asanteni
ALHAJ.
JAFARI KASISIKO MSAFIRI
WAMALWA
M/KITI
MKOA 01/DEC.2013 KATIBU
MKOA
0756439200 0786448443
0714439200 0756448442
CHADEMA MKOA KIGOMA
No comments:
Post a Comment