Tangazo

January 31, 2014

MAYOR JERRY SILAA KUBARIKI UZINDUZI WA KAMPUNI YA GRACING AFRICA LEO

1004083_796852693662558_866660999_n  
Mwanamitindo anayefanya vizuri sana nchini, Danny David atazindua kampuni yake mpya ya Gracing Africa inayojihusisha na ukuzaji na uendelezaji wa vipaji nchini hasa vya mitindo na fashion ijumaa hii katika hoteli ya Serena ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa meya wa jiji la Dar es Salaam mheshimiwa Jerry Slaa.

Uzinduzi huo wa aina yake utakuwa wa mwaliko pekee ni watu wachache watakaochaguliwa kuhudhuria sherehe hiyo.

Danny ambaye hivi karibuni amerejea nchini toka nchini Afrika ya kusini alipoenda kwa ajili ya shuguli za kizazi amesema lengo la kampuni hiyo ni kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wengi nchini katika lengo la kuboresha maisha yao.

January 30, 2014

MWILI WA SHEKH WA MKOA WA MARA WAWASILI UWANJA WA NDEGE MUSOMA

 NDEGE ILIYOBEBA MWILI WA MAREHEMU SHEKH ATHUMANI MAGEE

 MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIELEKEA KWENYE NDEGE KUONGOZA WAOMBOLEZAJI
 RUBANI WA NDEGE AKIELEKEZA NAMNA YA KUTOA JENEZA LENYE MWILI WA MAREHEMU


 NDANI YA GARI MAALUMU LA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA(JWTZ)LILILOBEBA MWILI WA MAREHEMU
 WAUMUNI WA DINI YA KISSLAMU PAMOJA NA WANANCHI WA MJINI MUSOMA WAKIWA UWANJA WA NDEGE
 AFIDH WAZIRI MMOJA WA WATU WALIOTOKA NA MWILI WA SHEKH MAGEE DAR AKIAGANA NA RUBANI WA NDEGE

 MWILI UKIONDOLEWA UWANJA WA NDEGE TAYARI KUPELEKWA NYUMBANI

 MSAFARA WA MWILI WA SHEKH MAGEE UKIPELEKWA NYUMBANI

 MKUU WA MKOA WA MARA NYUMBANI KWA SHEKH
 MWILI UKISHUSHWA NYUMBANI
 WAOMBOLEZAJI WAKIWA NYUMBANI
MKUU wa mkoa wa Mara Mheshimiwa John Gabriel Tuppa ameongoza maelfu ya Wananchi wa Mji wa Musoma kupokea mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa januari 28 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kugua kwa muda na mrefu na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Musoma wakiusubili mwili wa shekh Magee wamesema  wamepata pigo kubwa kutokana na msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza masuala ya dini.

Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa kesho kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.

   INNAH LILLAH WAINNAH ILLAH RAJIUUN
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA SHOMARI BINDA

UNIC yaendelea kutoa mafunzo ya mateso ya kambi za Wayahudi

DSC_0014
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.

Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania

Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.

“Ni muhimu kutoa mafunzo kwa vijana wakitanzania wa shule za msingi na sekondari ili wajue kwamba tofauti za rangi na za kidini hazina nafasi ya kutugawa kama binadamu,” amesema Nkhoma.
DSC_0005
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Diamond na Mlezi wao wakimsikiliza Bi. Ledama (hayupo pichani).
DSC_0044
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto.

Alisisitiza kwamba mauaji na mateso ya Auschwitz yalipoteza mamilioni ya watu wasio na hatia na mafunzo haya yanaonyesha chuki na ubaguzi dhidi ya wayahudi na chuki za aina nyingine yoyote hazina nafasi katika ulimwengu wa leo.

Nkhoma amesema kwamba binadamu wote ni sawa na tofauti za kipato au dini au rangi haziwezi tena kujenga chuki dhidi ya binadamu wengine kwa sababu wote kama binadamu tuna haki sawa mbele za mungu.
DSC_0051
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond jijini Dar es Salaam, wakifuatilia sinema maalum ya mauaji ya kambi za mateso ya wayahudi mwaka 1933.

Wakati huo huo, ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto amesema aliona makambi ambako wayahudi, waroma, wasinti, mashoga, wafungwa wa kivita na watu wenye ulemavu walitumia siku za mwisho katika hali ya kinyama.

“Umoja wa Mataifa ulianzishwa kuzuia kila aina hii ya fazaa kutokea tena, lakini bado misiba kuanzia Cambodia hadi Rwanda mpaka Srebrenica inaonyesha kuwa sumu ya mauaji ya kimbari bado inatiririka,” ilisema taarifa hiyo.
DSC_0082
Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond wakisoma baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa.
DSC_0077
DSC_0075

MO plans to build a USD 5 billion empire out of Dar

942331_578714148840668_773339795_n
.At the age of 38, Mohammed Dewji employs 24,000 people and claims to contribute 3.5% to Tanzania's GDP. Within the next 5 years, he plans to build a $5 billion empire out of Dar es Salaam.

by Kristin Palitza

What most entrepreneurs don’t achieve in a lifetime, he did in just over a decade. Mohammed Dewji single-handedly turned his father’s trading business into Tanzania’s largest import-export group. He grew Mohammed Enterprises Tanzania (MeTL) 30-fold and increased revenues from $30 million to $1.1 billion by diversifying into a multitude of sectors, including manufacturing, distribution, logistics, financial services, real estate, cement, energy and mobile telephony.

It’s not surprising that many people have a hard time imagining the humble beginnings Dewji comes from. His family, which stems from Gujarat state in western India and was blown in the proverbial dhow across the Indian Ocean, started out with very little. His grandmother opened a small trading shop, which she runs out of their home in Singida, a poverty-stricken town in central Tanzania. In this simple house, built from sand and mud, Dewji was born with the help of a traditional midwife.

“That wasn’t very smart. My mother and I almost died because I had the umbilical cord wrapped around my neck,” he recalls. But from then on, his fortunes changed.

His father, Gulam Dewji, who had by the mid-70s turned his mother’s shop into a flourishing import-export business, was able to sent his six children to good schools, first in Tanzania’s third-largest city Arusha and later in capital Dar es Salam. In their free time, Dewji and his siblings played tennis and golf.

“My father spent a lot of money educating us. He also believed sport creates discipline. He didn’t want us to just play a sport for fun. He wanted us to push ourselves. We probably have a thousand trophies at home that we won,” he says.

Until this day, there is almost nothing Dewji undertakes purely as a hobby. He either aims for success, or he doesn’t bother with it. And so he ploughs millions of Dollars into Tanzania’s national soccer team, the Taifa Stars instead of being content watching the odd game or kicking around a ball on a Sunday.

“I have no moderation. My wife always complains. She says, ‘Mohammed, why don’t you do things in the middle?’ It’s either very much or nothing at all,” he laughs.

His favorite sport has always been golf. Dewji spent many afternoons on Dar es Salaam’s golf course, not only because he was good it – he had 3 handicap – but also because he realized from early on that many high-profile business deals are concluded on the world’s 18-hole-lawns.
“I already liked to network as a very young guy. I was told that the golf course is a good place to meet important people. So I started playing golf. At one time, I even wanted to become a golf professional,” he says.

When his father saw that his son showed potential, he enrolled him at the legendary Arnold Palmer Golf Academy in Orlando, Florida, where Dewji also attended Saddlebrook High School. A few years later, when it became clear that Dewji wasn’t going to make the cut as a professional golfer, he decided to study international business and finance with a minor in theology at Georgetown University, an elite tertiary institution in Washington D.C., which has a long list of notable alumni, including former US president Bill Clinton, former Philippines president Gloria Arroyo and Jordan's King Abdullah.

During his time at Georgetown, Dewji learned what he says were key lessons in leadership. “Georgetown really molded me. It took me a step forward. I understood that you need to be dreaming, but not daydreaming. You need to try to dream a reality. Then you have vision,” he explains.

Pietra Rivoli, deputy dean of Georgetown University’s school of business, who taught Dewji in international finance, remembers him as a student whose energy was boundless and whose positive enthusiasm was contagious.

“While other students tried to stay awake through discussions of exchange rates, Mohammed would stay after class to talk about how the readings might pertain to the Tanzanian Schilling, and how Tanzania could address its economic challenges. Even at the age of 20 or so, he was thinking about how to improve life in his country,” she remembers.

Dewji never questioned if he should return to Africa after his graduation in 1998. He joined his father’s business, which had by then become a million Dollar trade and transport group, as chief financial controller. Five years later, at the age of 29, he was promoted to managing director, expanding his father’s business hard and fast. “I went into manufacturing and value-addition. I built a distribution system and created branches,” he says.

Today, MeTL Group is buying and selling more than 200 commodities in east, central and southern Africa, from sugar to rice, salt, fertilizer, second-hand clothing, motorcycles, bubblegum, yeast and ballpoint pens. The group also distributes 50 of its own brands, taking advantage of the fact that Tanzania borders on eight countries and is thereby an ideal import-export gateway.

“The goods that I am mainly dealing in are FMCGs [fast moving consumable goods]. It’s goods that touch people’s lives, that are needed by the common man,” he says.

The distribution of FMCGs is not an easy task in a vast country like Tanzania, which measures a million square kilometers and where 80% of the population lives in remote, rural areas. But with more than a hundred trade outlets countrywide, MeTL Group has managed to undercut multi-national consumer goods giants like Unilever and drive them out of the east African nation.

“I have a big basket of goods. I have warehousing and logistics. I have over a thousand trucks. It’s all complimenting each other. It’s very difficult for people to come from the outside and compete with me,” Dewji explains.

He invests in whatever sector he sees opportunity and growth potential. Or to say it differently: the only two industries Dewji is not involved in are beer and tobacco.

Agriculture is another key sector for MeTL Group, which with a workforce of 24,000 people is also the country’s biggest employer, and with 50,000 hectares of arable land, the largest private landowner. Dewji’s sisal farms, tea gardens and cashew fields are the drivers of his FMCG export business. A good 99% of the cashew kernels he produces, for example, are shipped to the United States.

Always thinking two steps ahead, Dewji has been making plans for how to profit most from his land, while helping to solve the challenges of Dar es Salaam’s rapid urbanization, a city of 4.4 million people. He is busy turning a 17,000 acre plot he bought cheaply several years ago, just 25 kilometers outside of the capital, into a dry-port with an internal container depot and a railway connection that will feed into Dar es Salaam’s massive, natural harbor, which is slowly but surely running out of space. It will, of course, also generate huge profits.

Since MeTL Group already contributes 3.5% of Tanzania’s GDP, it is fast outgrowing national boundaries.

“If you compare, for example, Tata and the MeTL Group, we are like Mickey Mouse. But if you look at their contribution to India, vis-à-vis my contribution to Tanzania, mine is bigger. You end up competing with everybody in your own country, and I don’t think that’s healthy. It’s a risk area. It’s a good time for us to replicate what we are doing in Tanzania in other countries,” he explains his expansion plans.

A workaholic at heart, Dewji never thinks small. “Slowly, slowly, I am planning to take on the whole continent. I am very bullish,” he says about himself. His five-year-plan is to turn MeTL Group into a $5 billion empire.

“We have to constantly revisit our visions, because we are outgrowing them so quickly. Who would have thought we could turn our business from $30 million to $1.1 billion in only 12 years? I believe that by 2018, we will be a $5bn business. Easy. It’s a no-brainer. If you look at the business we are in and the growth potential that there is, it’s amazing. My philosophy as a businessman is not to be satisfied with what I have got, but to always work harder to achieve more,” he says.

It’s been quite some years now that MeTL Group, under Dewji’s helm, has expanded so drastically that it has outgrown the loan potential of Tanzania’s banks. Dewji has found a solution to this problem, too. He goes to one of the continent’s powerhouses, South Africa, to finance new ventures. Most recently, he secured a $100 million syndicated loan through a grouping of banks.

“If I think of a top African businessman, Mohammed comes to mind. He works very long hours, is always on the move, has an eye for opportunity and a very good business sense. He is levelheaded and pays extremely close attention to detail,” says Helmut Engelbrecht, head of Investment banking in Africa at Standard Bank, one of the financial institutions that has been working closely with MeTL Group.

Whatever venture Dewji pursues links closely into his country’s national policy framework. When Tanzania’s government launched a national strategy for economic growth and poverty reduction in 2005 that was geared, among other things, towards boosting entrepreneurship to achieve value addition and employment creation, Dewji immediately saw opportunity.

“I bought a lot of sick industries, including soap production, grain milling, rice and sugar blending. I also went into the edible oil business and the textile industry,” he says.

He first expanded MeTL Group’s edible oil refining capacity from 60 to 600 tons. This year, Dewji almost quadrupled the business when he purchased an additional 1,650-ton refinery, increasing his total output to 2,250 tons of edible oil. It comes as little surprise that he has caught the attention of some of Africa’s wealthiest investors.

“I am being approached by many big boys, by multi-national companies that want to partner with me or buy me out. But I am not ready to sell yet. I can see so much more opportunity for growth. I don’t want to be paid based on what I am earning today, because I can see the tremendous potential. I am always looking five, ten years ahead,” he explains.

Another ailing sector Dewji rescued is Tanzania’s textile industry. Knowing that the east African nation is the continent’s third largest cotton producer, he decided to buy and refurbish four run-down mills, three in Tanzania and one in Mozambique. His next step will be to move into Zambia and Malawi, he says, considering Ethiopia as a potential fifth standpoint.

“We were quite lucky. Tanzania’s previous, socialist government had invested hundreds of millions of Dollars in infrastructure to build textile mills. But under socialism everything collapsed. So we were able to acquire these industries very cheaply. Obviously the machinery was all run-down, the technology obsolete. We had to rehabilitate the mills by investing in top European and American machinery,” says Dewji.

He has turned MeTL Group into sub-Sahara Africa’s largest textile player, integrating the entire value-addition chain from ginning to spinning, weaving, processing and printing.
“This year, we are going to produce more than a hundred million meters of cloth. That is more than 2,500 times the circumference of the earth,” Dewji says with pride.

Due to his entrepreneurial vigor, Tanzania is able to compete with the world’s largest and cheapest textile producer, China – at least within its own borders where government policies, including import tariffs on textiles and a standard value added tax (VAT) of 18% help protect the industry.

“Today, overall textile production is cheaper in Tanzania than in China. Labor is competitive in terms of pricing. Tanzania’s big advantage is that we have cotton, while China has to import cotton. So they cannot compete with me in my market,” Dewji explains.

His success speaks for itself. This year alone, he will earn at least $85 million after taxes, he says. But he is far too humble to take credit for the entirety of his achievement.

“People often ask me: ‘Who is smarter, you or your father?’ I ask them back: ‘Is the person who goes from zero to ten smarter, or someone who goes from ten to a thousand?’ Obviously, it’s much easier to go from ten to a thousand than to start from zero. So I believe that my father is much smarter than me,” he says.

Nothing could be further from his mind than taking it easy, or even early retirement.
“People in Tanzania look at my wealth and think I must be sunbathing and playing golf all day. But I work really hard. I put in a hundred hours a week. It’s a never stopping game. You can never say, ‘I’ve worked hard enough now’,” says Dewji, who has 60 divisional board meetings every month, or two per day.

Every morning, Dewji, who lives in with his wife, daughter and two sons in one of Dar es Salaam’s best neighborhoods, starts work at 6AM, spending the first hour responding to emails and reading commodity reports. He then runs meetings until lunch, by which time he has already put in almost seven hours of work.

“When I feel my energy levels starting to drop, I drive to the gym near my house. Every day, I run three kilometers and lift weights. I like to keep fit,” says Dewji, who is of slender built and the proud owner of a ‘six-pack’.

After gym, he goes home for lunch and to play 15 minutes with his three children before he returns to the office until late at night. The only days he takes off are Sundays, he says, when he spends time with his family and totally shuts off from work.

“Until about four years ago, I also used to work on Sundays, until my wife almost divorced me,” he jokes. 

Dewji is not only growing his own empire. He is putting Tanzania on the map, making sure the east African nation – which boasts the continent’s third largest gold reserves, recently discovered uranium and gas reserves as well as a flourishing tourism industry combined with long-term political stability – will become one of sub-Sahara Africa’s big economic players, together with South Africa, Nigeria, Ghana and Kenya.

Already, Dar es Salaam is the second fastest growing African city after Lagos. And Tanzania, which boasts an average of 7% national economic growth over the past decade, has become one of the fastest growing economies in the world. According to World Bank, Tanzania’s per capita GDP more than doubled from $730 in 2000 to $1,500 in 2012.

“There’s no doubt that the country’s purchasing power is increasing,” notes Dewji, who believes the whole of sub-Saharan Africa, which currently has an overall growth rate of 4.8%, could achieve double-digit growth figures if countries are well-governed, politically stable and create conducive environments to attract investment.

As if Dewji didn’t already have enough on his plate, he is also in politics. The decision was made when he visited Singida, the town and district he grew up in, after returning from the US. As he walked the city’s streets, he encountered an old man who was scooping yellowish water out of a dirty puddle. It was his family’s only access to drinking water.

“A lot of people die from water-born diseases in rural Tanzania. But every life has the same value. So I decided to run in the next elections to change the dire situation these people live in. I was 24 years old. My parents thought I was crazy,” he remembers.

Whatever Dewji sets his mind to, he turns into a success. In 2005, he was elected as a Member of Parliament in the National Assembly of Tanzania. Five years later, he was re-elected in a landslide victory with 80% of votes. Not being a fan of ‘politicking’, Dewji, who is fluent in both English and Kiswahili, says he decided to put his own spin on the role of an MP.

“I don’t really have time for politics. I don’t go to parliament, and I don’t get involved in national politics, because I don’t want it to conflict with my business interests. All I do is serve my constituency because I believe people see hope in me,” he explains.

He puts his money where his mouth is. Every year, he donates half a million Dollars of his own money to help the people of Singida, with focus on three areas: education, health care and water. And with tangible success. In years Dewji has been representing the central Tanzanian district, access to clean water has jumped from 23% to 75%, while the number of secondary schools increased from two to 18.

“I studied theology as a minor because I feel that religion is complimenting me. It makes you strive to become a better person. I am very conscious of everything I do. If you get too engrossed in making money, you lose focus on life. Life is very short. I don’t want to die with all this money,” he explains.

Even though he makes millions, he has little interest in living a life of utter luxury, employing only a driver, a butler and private security.

“You have to live well, but you don’t have to live lavishly to the extreme. You need to be humble. I could buy a plane, a Rolls Royce or a Bentley. But I don’t. If drilling a borehole costs $20,000, you tell me to buy a watch for $20,000? To make a decision that has an impact on people’s lives is a one-second decision for me. If you get too egocentric, you lose your vision. It deceives you.”

January 29, 2014

THIS SATURDAY @ISUMBA LOUNGE(JOLLIES CLUB) W.V.B dress in white v/s black with the LEGENDS karibu sana.


KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 37:CCM YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.
######################################

   Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka 1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa  Watanzania ,kutunza na kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa nchi,akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  alisema  sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.

  Kilele cha sherehe hizi  kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa nini tarehe mbili na sio tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”
Sherehe hizi zitahitimishwa hapa jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na kesho anategemewa kuwasili Makamu Mwenyekiti  wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet  Mangula ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya  akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama ,Rais Jakaya mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.
Wakazi wa Mbeya waombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi  tarehe moja na pia washiriki kwenye matembezi na sherehe zitakazofanyika tarehe2.

Maadhimisho ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali mbali nchi kote ,ikiwa pamoja na shughuli  za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti,kushiriki shughuli za maendeleo kujenga shule na zahanati,usafi  pamoja na kutembelea wagonjwa hospitalini.

Uchaguzi Mkuu wa Taswa Februari 16 mwaka huu

Amir Mhando

UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), utafanyika Februari 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam kama ulivyopangwa na Kamati ya Utendaji ya chama.

Hata hivyo sekretarieti ya TASWA imekubaliana kusogeza mbele muda wa kulipia ada kwa wanachama hadi Jumanne Februari 4 mwaka huu, badala ya Ijumaa Januari 31, 2014 iliyokuwa imepangwa awali, lengo likiwa ni kuwezesha wanachama wengi zaidi kulipia ada zao ili waweze kushiriki uchaguzi huo.

Wanachama wote walioshiriki uchaguzi wa mwaka 2007 ama 2010 au Mkutano Mkuu wa mwaka 2012 wana sifa ya kushiriki uchaguzi huo wanachotakiwa kufanya ni kulipia ada zao kuanzia mwaka 2011.

Malipo yafanywe kwa Mhazini Msaidizi, Mohammed Mkangara, 0658-123082 na hakuna mwanachama mpya atakayekubaliwa kujiunga na chama kwa sasa mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu.

Nawasisitiza wanachama kuhakikisha wanatumia vizuri muda uliobaki kwa kulipia ada zao ili waweze kushiriki mkutano huo. Kamati ya Uchaguzi ya TASWA inatarajiwa kukutana Jumatatu ijayo kuzungumzia mambo mbalimbali yahusiyo uchaguzi huo.

 Imetolewa na:

 Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
29/01/2014.

NAPE AJICHANGANYA WA WANANCHI SOKO LA MWANJELWA MBEYA

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akicheza draft na vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya.
Nape yupo mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambazo kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.Katibu wa NEC alikutana na vijana mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa pamoja nao kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM zilizoimbwa na Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana na baadhi ya madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula cha mchana kwenye kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.
 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia mechi ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya mpira kati ya timu ya soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua Mabelo kwenye uwanja wa mpira wa sokoni Sido.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya mara baada ya mpira kumalizika.

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YAPAMBA MOTO

 Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Luteni Mstaafu Maganga Sengelema akifafanua jambo mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ikiwa sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambayo kitaifa mwaka huu inafanyika mkoani Mbeya.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Maganga Sengelema akimuonyesha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye sehemu ya kuweka jukwaa la waandishi wa habari kwenye uwanja wa Sokoine ambapo sherehe za miaka 37 ya CCM zitasheherekewa kitaifa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa maandalizi ya awali katika uwanja wa Sokoine ambao unategemewa kufanyika kwa sherehe za mika 37 ya CCM tarehe 2 mwezi wa februari mwaka huu,mgeni wa heshima anategemewa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kurekebisha uwanja wa Sokoine ili uweze kutumika vizuri wakati wa sherehe za miaka 37 ya CCM . Picha na Adam H. Mzee

January 28, 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA KONGAMANO LA KILIMO AFRIKA MASHARIKI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kitabu cha Mandela toka kwa Mkurugenzi wa Programu wa Spintelligent ya Afrika Kusini Bi. Amore Swart baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Bi Meab Mdimi wa Kampuni ya Kilimo ya TECHNOSERVE  baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo katika banda la Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Kusini mwa Ukanda wa Afrika (SAGCOT)    baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014. PICHA NA IKULU

TAMKO LA JUMUIYA YA VIJANA KUUNGA MKONO KAZI YA SEKRETARIETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CHINI YA KATIBU MKUU NDUGU ABDULRAHAMAN KINANA

Paul Makonda
“Inapofikia wasimamizi wa Kanuni za Chama wanapigwa vita ya wazi kwa uamuzi wao wa kukisimamia Chama, tafsir yake ni moja tu watu wanaowapiga vita hawakitakii mema chama chetu.”

“..Chama Cha Siasa chochote  duniani hubomoka kutokana na migongano iliyokithiri ya muda mrefu. Uzoefu wa vyama vikubwa vilivyoporomoka umeonyesha hivyo!  Chama lazima kidhibiti uchu wa madaraka wa baadhi ya viongozi wake na ndani ya serikali yake...” – Dr Eginald P. Mihanjo

“..Chama cha siasa ni itikadi. Chama cha siasa ni siasa kwa maana halisi ya neno lenyewe siasa –“siasa”. Ni mahali ambapo watu wenye madhumuni mamoja yaliyoainishwa waziwazi hukutana na kuwa kitu kimoja.  Chama cha siasa sio mkusanyiko wa “majini dume yenye tamaa”, - majini ambayo yametanguliza mbele tamaa kufa na kupona-tamaa ya kutengeneza pesa au kupata vyeo kwa gharama   yoyote! – Dr Bashir Ally



UTANGULIZI:
Hili ni tamko la vijana makini wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuunga mkono juhudi na utendaji wa sekretarieti ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi ikiongozwa na Katibu Mkuu Komredi Abdulrahaman Kinana.

Maneno ya utangulizi yamebeba dhima ya tamko hili, kufuatia taarifa zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari vikiwanukuu baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi,wakiwatuhumu Viongozi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahaman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Ndugu Nape Moses  Nnauye.

Sisi Vijana tunatambua kuwa tuhuma hizo na maneno hayo ya hovyo yametolewa kwa nia ovu yenye kulenga kuwakatisha tamaa Viongozi hao wa Chama. Tunafahamu kuwa upo mkakati wa kiuhaini ulioandaliwa na kuratibiwa na “mtandao” ndani ya Chama ambao umejipanga kuendesha uhaini huo.

Sisi vijana wa UVCCM tunatambua na kuthamini juhudi za Katibu Mkuu na Sekretarieti yake katika kukijenga na kukiimarisha Chama kwa kuisimamia barabara misingi na shabaha ya kuundwa kwake, katika umri wetu hatukuwahi kuona Chama kikiwa karibu na wananchi kwa kufuatilia, kusikiliza na kushiriki katika utatuzi wa kero, shida na changamoto zao kama ilivyo katika kipindi hiki chini ya Comrade Kinana na timu yake. Juhudi hizi ni za kuungwa mkono na kamwe si za kubezwa na mwanaCCM muadilifu, muaminifu na mwenye mapenzi ya kweli kwa Chama.

Juhudi za kukiimarisha Chama kutoka ngazi za chini, kwa mabalozi ni mkakati bora kuwahi kutekelezwa na Chama, kukirudisha Chama kwa wanachama ni kutimiza lengo la kuundwa kwa Chama hiki, Chama hiki ni cha wanyonge, masikini wa Taifa hili, HAIWEZEKANI matajiri watake kukihodhi na waratibu mikakati ya kukihujumu kwa pesa zao hali sisi vijana tukitazama, tunasema tutakilinda Chama chetu na tutawalinda viongozi wetu waadilifu.

Ni hawa ambao wanabezwa leo ndio wameweza kurudisha Imani ya wananchi kwa Chama, Imani na matumaini ambayo tayari yalishaanza kupotea na Chama kuonekana si tena cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi wa nchi hii.

Ni Comrade Kinana na timu yake ndio waliozunguka kwenda kukutana na wakulima wa Pamba kule mikoa ya Kanda ya ziwa na kumpeleka balozi wa China na kumshawishi kujenga viwanda ili kuboresha manufaa kwa wakulima.

Ni Comrade Kinana na timu yake ndio waliokwenda Kusini kukutana na wakulima wa Korosho na kushirikiana nao pamoja na bodi kutatua tatizo la Korosho.

Ni Comrade Kinana na timu yake ndio walioibua hoja na kero za wafugaji, walimu na wananchi kwa ujumla, na kuwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanawajibika kwa wananchi walipa kodi wa Taifa hili.

Kupinga mafanikio ya Ziara hizo ni kupinga utetezi wa wanyonge.

Mtu anayebeza ziara hizo na kuwaita Viongozi waliozifanya waropokaji na wahuni wahuni ni mtu mjinga, mtu wa hovyo,hana maadili, asiyekipenda Chama, mhaini na mzandiki anayepaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.

TAMKO hili limezingatia wosia wa Baba wa Taifa, muasisi wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Julius Kambarage Nyerere katika kitabu Chake TUJISAHIHISHE.


Imetolewa na Paul Makonda.

Katibu wa Hamasa na Chipukizi.

MATUKIO YA RAIS IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi ya timu ya baseball ya Chicago Cubs  toka kwa mmiliki wa  timu hiyo na Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea  moja ya Tabuleti 61  kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani    toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014. PICHA NA IKULU

VIDEO: MOHAMMED ENTERPRISES TANZANIA'S EXPANSION PLAN IN AFRICA

BeqsooUCAAIEJjg
The World Economic Forum brought together political, business and civil society leaders to discuss economic development issues. It also attracted a host of entrepreneurs, among them Forbes' youngest member of the rich list, Mohammed Dewji, Group Chief Executive Officer of Mohammed Enterprises Tanzania. CNBC Africa's Bronwyn Neilson spoke with him about the company's expansion on the continent.

Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama yapewa msaada wa dola laki moja kwa ajili ya udhamini wa wanafunzi wa kike shuleni hapo

Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakipokea moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa  Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.
#########################
Na Anna Nkinda – Maelezo
 Taasisi ya Fursa ya  Elimu (Opportunity Education Foundation) ya nchini Marekani imetoa mchango wa dola za kimarekani laki moja kwa ajili ya udhamini wa wanafunzi wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi katika shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama iliyopo wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.Fedha hizo ambazo ni zaidi ya shilingi milioni mia moja na  sitini na mbili  zitaweza  kuwasomesha wanafunzi 75 kwa kipindi cha mwaka mzima kwa kuwapatia malazi, chakula, sare za shule, viatu, shajara, vitabu na mahitaji mengine ya kila siku ya mwanafunzi.
 Hayo yamesemwa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ambao ndiyo wamiliki wa shule hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa laptop ndogo (tablets computer) uliofanyika shuleni hapo jana. 
 Mama Kikwete pia alimpongeza  Joe Ricketts ambaye ni mwanzilishi na mtendaji mkuu wa Fursa ya  Elimu kwa moyo wa upendo alionao na dhamira ya kuisaidia jamii ya watanzania kwa kutambua kwamba kupata elimu bora kwa wanafunzi wote ni ufunguo wa kuwa na afya bora, uchumi imara, miundombinu bora na ya kutosha, jamii yenye uelewa jambo ambalo litasababisha ustadi wa taifa kunasonga mbele.
 Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema , “Kwa mantiki hiyo ningependa kusema kwamba kukosekana kwa fursa ya kumpatia mtoto wa kike elimu bora ni kulikosesha taifa fursa ya maendeleo kwani kadri mtoto wa kike anavyopata elimu ndivyo anavyoweza kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na ataweza kuboresha uzazi wa mpango, afya ya mtoto na kujiongezea kipato”.
 Akizungumzia kuhusu mradi wa laptop ndogo (tablets) ambapo shule hiyo ilipata 61  Mama Kikwete  aliiomba Taasisi hiyo na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuangalia uwezekano wa kuongeza mitaala ya mafunzo ya kitanzania ili iwasaidie wanafunzi kumudu masomo wanayofundishwa darasani halikadhalika kuandaa mkakati wa kuzifikia shule zilizopo pembezoni ambazo zinakuwa na uhaba wa walimu.
 “Ninawaasa walimu na wanafunzi wa shule hii na kupitia wanafunzi wa shule zitakazofaidika na mpango huu kutumia vifaa hivi kwa mahitaji ya masomo kama ilivyokusudiwa na siyo kupoteza muda kwa michezo isiyo na manufaa. Napenda mjione kama watu wenye bahati ambao mmepata fursa ya kipekee ambayo wanafunzi wengi nchini hawana, mvitunze vifaa hivi ili viwafae wanafunzi wengine watakaokuja baada yenu”, alisisistiza Mama Kikwete.
 Kwa upande wake Ricketts alisema kwa mara ya kwanza alikuja nchini mwaka 2006 wakati anaelekea   Serengeti alikuta mwalimu mmoja anafundisha wanafunzi zaidi ya miamoja aliamua  kuanzisha  mahusiano na shule hiyo ambayo aliwapelekea vifaa mbalimbali vya kufundishia.
 Alisema lengo la  kuanzishwa kwa Taasisi yake ni kutoa msaada wa kielimu ikiwa na nia ya kufanya upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi kutoka nchi zinazoendelea ili wale wanaotoka katika familia maskini waweze kusoma na kupata ajira pale watakapokuwa wamemaliza masomo yao na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
 “Vijana wadogo wanategemea kupata elimu bora kwa kuwa  elimu kwa wanafunzi imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni technolojia na mwanafunzi mwenyewe kukuwa na kukomaa kiakili ili aweze  kufanya vizuri katika masomo yake.
 Kama mradi huu utafanikiwa walimu watakuwa na mwamko mkubwa wa kufundisha na nitahakikisha kuwa zinapatikana laptop ndogo (tablets) za kutosha kwa ajili ya kusomea nchini kwani matokeo ya maisha ya watoto  wetu yanategemea elimu wanayoipata” , alisema Ricketts.
 Taasisi ya Fursa ya  Elimu ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa nchini mwaka 2006 walianza kufanya kazi na shule moja ya msingi na hadi kufikia sasa  shule 434 zikiwemo za Sekondari 33 zimenufaika kwa kupata vitabu, DVD na zana za kufundishia.
 Kwa shule za sekondari wanatoa mwongozo wa mwalimu ambao unamuongoza kirahisi jinsi ya kuwafundisha wanafunzi , laptop ambazo zinamasomo yaliyorekodiwa ambayo ni ya sayansi, hesabu, kiingereza na maarifa ya jamii ,projecta na Televisheni ambazo zinasaidia kuonyesha masomo na vitabu na video inawasaidia wanafunzi kujifunza somo la kiingereza kwa njia ya kusikiliza na kusoma.
 Wanafunzi watakaonufaika na program hiyo ni wa kidato cha pili kutoka  shule za Sekondari Ilboru,(Arusha) Mzumbe (Morogoro),  Msalato, (Dodoma),FidelCastro (Pemba), WAMA - Nakayama (Pwani), shule ya Sekondari ya wavulana Bwiru (Mwanza), J Ossian (Bukoba), Laureatte (Zanzibar), Notredame (Arusha) na Tusiime (Dar es Salaam).