Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya
mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (kushoto)
akikabidhi masaada wa unga wa sembe kwaajili ya uji wa wanafunzi shule ya
msingi Levolosi. Wanao pokea ni Mwenyekiti Kamati ya Shule, Edward Ngomuo
(kulia) Mwalimu Mkuu Shule ya Luvolosi, Elisante Kaaya na Mwalimu wa Chakula
shuleni hapo, Frida Mallya.
*********
JAMII imetakiwa kuwa na moyo wa kujitolea na kusaidia makundi
mbalimbali yenye uhitaji katika jamii hasa wanawake na watoto ili kujenga
taifda lenye matumaini na amani.
Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine
Foundation, ya jijini Arusha, Catherine Magige wakati akikabidhi msaada wa unga
wa sembe na sukari kwaajili ya kuwapikia uji wanafunzi zaidi ya elfu moja katika
shule ya Msingi Levolosi ya mjini hapa kwa muda wa mwezi mmoja.
Magige ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM) mkoa wa Arusha,
amesema kila mtu anapswa kujipima kwenye mizani ya ubinadamu, kujitafakari na
pia kujiuliza maswali magumu kwenye nafsi yake, kwamba, katika kipindi kifupi
cha uhai wake, ameacha nyuma matunda ya aina gani.
“Tunapaswa tusambaze mbegu za matunda ya amani na upendo na si mbegu
za machafuko…kwani ndio mbegu ambazo sote tunapaswa kuzisambaza na kuzipanda
ili kujenga taifa lenye matumaini na amani,”alisema Magige.
Ni ukweli usio pingika kuwa watoto wetu hawa tusipo wawezesha
kupata elimu sasa basi tutakuwa tumejingeneneazea wenyewe taifa la watu
mbumbumbu na wasio na ujuzi wa kufanya jambo lolote jema na matokeo yake
wataishia katika magenge ya uhalifu na watumiaji wa madawa ya kulevya.
Magige amesema ili watoto wafanye vizuri darasani wanahitaji
kushiba na si familia zote zinamudu kuwapa chakula watoto wao kabla ya kwenda
shule hivyo taasisi yake ya Catherine Foundation imeona ichangie kulisha watoto
hao kwa mwezi mmoja.
“Sisi kama wazazi hatuna budi kusaidia wazazi wengine ambao
wanania njema na watoto walio wazaa isipokuwa uwezo ndio unawakwamisha katika
kutimiza malengo yao ya kuwasaidia watoto wao katika elimu,” alisema Magige.
Aidha amesema utaratibu wa kuwapa watoto chakula shule utaongeza
kiwango cha usikivu wa wanafunzi darasani na kuongeza ufaulu huku ukupunguza
tatizo la utoro mashuleni ambalo limekithiri katika shule nyingi nchini.
“Kufanya hivi situ watoto watakuwa wasikivu darasani bali hata
kuchangia kwa kiwango cha ufaulu darasani na ni wazi kuwa hata mahudhurio
yataongezeka shuleni hapa,” alisema Magige.
Pia amewataka wanafunzi wanafunzi kukazania masomo yao darasani,
kudumisha nidhami mingoni mwao huku akiwataka walimu kutimiza wajibu wao
ipasavyo kwa kuwapa elimu bora na malezi stahiki watoto hao na maadili mema.
Mapema katika hotuma yake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi
Levolosi, Elisante Kaaya alisema shule hiyo ina wanafunzi 1,029 na gharama za
kuwalisha kwa mwaka zinakadiriwa kuwa zaidi ya Sh Milioni 10.
Aidha Mwalimu Kaaya alisema kuwa ili kufanya zoezi hilo la kuwapa
uji au chakula wanafunzu linaendelea wameazimia kuwashirikisha wazazi na wadau
wengine wa elimu ili uwe endelevu na wenye kuleta tija.
Ofisa wa Catherine Foundation Lucy Bongole akizungumza jambo kabla ya makabidhiano kuanza.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi
Levolosi, Elisante Kaaya akitoa maelezo ya shule hiyo na mpango wa kuwapa uju wanafunzi wanafunzi 1,029 na gharama za
kuwalisha kwa mwaka zinakadiriwa kuwa zaidi ya Sh Milioni 10.
Juice zikigawiwa kwa wanafunzi.
Mwenyekiti wa Shule ya Msdingi Levolosi ya jijini Arusha, Edward Ngomuo akisema neno.
Mwenyekiti wa Catherine Foundation na Mbunge wa viti Maalum Arusha, Catherine Magige akigawa juice kwa wanafunzi.
Mwenyekiti wa Catherine Foundation na Mbunge wa viti Maalum Arusha, Catherine Magige akizungumza.
Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya
mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (wapili
kushoto) akimuweka katika kiti maalum cha magurudumu, motto mlemavu Hassan
Ramadhani (10) mkazi wa Luvolosi mjini Arusha jana. Wanaoshuhudia ni mama mzazi
wa motto huyo, Hadija Hassan na Mwalimu Mkuu Elisante Kaaya wa Shule ya Msingi
Luvolosi.
Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya
mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (kushoto)
akikabidhi masaada wa unga wa sembe kwaajili ya uji wa wanafunzi shule ya
msingi Luvolosi ya mjini Arusha jana. Anaeshuhudia ni Mwalimu Mkuu Elisante
Kaaya.
Wazazi na walimu wakipokea unga na sukari
wanafunzi nao wakipokea
Wawakilishi wa wazazi wakipokea msaada huo.
Mwalimu wa Chakula
shuleni hapo, Frida Mallya akitoa neno la shukrani kwa taasisi ya Catherine Foundation.
Mwenyekiti wa Catherine Foundation, Catherine Magige akiagana na wanafunzi.
No comments:
Post a Comment