Afisa
Uhusiano wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania Jane Matinde,
(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu
PhilemonNathaniel Mgaya aliyejishindia shilingi milioni tano (5m/-)
ikiwa ni zawadi ya wiki katika promosheni ya Mimi ni Bingwa.
Makabidhiano hayo yalifanyika mwishini mwa wiki katika ofisi za makao
makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
**********
Na Mwandishi Wetu.
MKUU
wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu PhilemonNathaniel Mgaya anakila sababu
za kuwa na furaha baada ya kuibuka mshindi wa shilingi milioni tano
(5m/-) za Airtel Tanzania Mimi ni Bingwa promosheni zinazotolewa kila
wiki.
Hili
linakuja wakati bado wiki chache tu kampuni hiyo ya mawasiliano
kutangaza mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 ambaye
atapatikana katika kilele cha promosheni hiyo.
Akizungumza
wakati wa droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Jane Matinde, Afisa
Uhusiano wa Airtel Tanzania alisema matokeoi mazuri ya promosheni hiyo
inadhihirisha dhamira na jitihada za kampuni za kuwasaidia wateja wake.
“Airtel
kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa leo hii inaendelea kuzawadia
wateja wengine, tukielekea katika droo kubwa ambayo itachezeshwa hivi
karibuni, droo itakayomwezesha mshindi mmoja kuondoka na kitita cha
shilingi milioni 50.
“Philemon
Nathaniel Mgaya ambaye anapokea hundi yake leo hii, ni mmoja kati ya
washindi wetu wa kila wiki aliyejishindia shilingi milioni 5 katika
promosheni hii iliyobadilisha maisha ya watanzania wengi.
“Tangu
promosheni ya Mimi ni Bingwa ianze katikati ya mwezi Novemba mwaka
jana, tumeona watanzania wengi wakishinda kila siku na kila wiki. Airtel
kupitia Airtel Money imekuwa ikihakikisha wanaojishindia zawadi za
chini ya shilingi milioni 5 wanapokea pesa zao ndani ya masaa 24 bila ya
kukatwa garama za kutoa, wakati wale waliojishindia shilingi milioni 5
wanapata pesa zao kupitia akaunti zao za benki,” alisema Jane.
Alisema
kuwa wateja wote wa Airtel bado wananafasi ya kujishindia milioni 50
pesa taslim, kutokana na kuwa mshindi atapatikana kupitia bahati nasibu.
“Kwa
mujibu wa vigezi na masharti ya promosheni, kila namba iliyojisajili
kwenye promosheni, hata kama mteja amejibu swali moja tu, atakuwa
ameingia kwenye droo kubwa.
“Huu
ni wakati sasa wa wateja wengine wa Airtel ambao hawajajisajili kwenye
promosheni waingie kwenye promosheni kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye
neon “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo,
unaweza kuwa mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50,” alisema
Jane.
Mara
baada ya kupokea hundi yake ya shilingi milioni 5, Philemon Nathaniel
Mgaya alisema pesa alizopokea zitamsaidia kutanua biashara yake
aliyoianzisha baada ya kustaafu kazi katika Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment