Tangazo

February 13, 2014

TIB NA DBSA ZAINGIA MKATABA KUKOMBOA SEKTA YA UCHUKUZI NCHINI

 Mkurugenzi wa Mipango Mikakati wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Jaffar Machano akifungua mkutano huo wa hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano.
********
Nwa mwandishi wetu,
Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank) na Benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Development Bank of Southern Africa, DBSA) zimeingia mkataba wa makubaliano ya kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini jana jioni.


Makubaliano hayo yatasaidia kufufua miundombinu ya uchukuzi ikiwemo Reli ya Kati, Viwanja vya Ndege vya Arusha na Mwanza pamoja na Upanuzi wa Bandari.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana jioni.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Peter Noni akizungumza na wadau wakati wa hafla hiyo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (DBSA), Patrick Dlamini akizungumza na wadau katika hafla hiyo.
 Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Kiserikali,Bunge na Binafsi wakifuatilia matukio ya hafla hiyo.
 Kutoka kushoto ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick Dlamini, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Peter Noni wakifuatilia kwa makini sehemu ya matukio wakati wa hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimani nchini (TIB Development Bank), Peter Noni (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick Dlamini (wa pili kushoto) wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi huku ukishuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia waliosimama) na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia waliosimama). Kushoto (waliokaa) ni Meneja Mkuu wa Fedha wa DBSA, Bane Makene na Mwanasheria wa Bodi ya TIB Development Bank, Martha Maeda (kulia). 
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimani nchini (TIB Development Bank), Peter Noni (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick Dlamini (wa pili kushoto) wakibadilishana nyaraka baada ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Fedha wa DBSA, Bane Makene na Mwanasheria wa Bodi ya TIB Development Bank, Martha Maeda (kulia).
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe wakizungumza na washiriki wa hafla hiyo.

No comments: