Tangazo

March 29, 2014

MBUNGE WA NZEGA, DK. KINGWANGALA: TCME WAMEUPOTOSHA UMMA

SINDA ISLAND TOUR


RIDHIWANI AITEKA PERA

Mwananchi wa Kata Pera waahidi kumpigia kura Ridhiwani Kikwete tarehe 6 mwezi wa nne baada ya kuridhishwa na Hotuba zake zinazogusa changamoto zao kama elimu, maji, zahanati, barabara na namna atakavyoboresha miundo mbinu ya jimbo la Chalinze na kuwasaidia wafugaji katika suala zima la kuongeza majosho ya mifugo.

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete  akihutubia wakazi wa kijiji cha Pera wakati wa mkutano wa kampeni za Ubunge Jimbo la Chalinze, Ridhiwani aliwaambia wananchi hao kura yao ya tarehe 6 mwezi wa Nne itakuwa ndio jibu la changamoto zote kwa wananchi wa jimbo la Chalinze kwani anatambua Changamoto zote za jimbo hilo.
 Imani Madega akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Pera na kuwataka wana CCM kuwa kitu kimoja na kuhakikisha Ridhiwani Kikwete anashinda kwa kura nyingi ilikufanikisha azma ya kusaidia jimbo la Chalinze kukua kimaendeleo inakua.
 Msanii Sam wa Ukweli akiruka juu na Morani wa Kimasai wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge kupitia CCM uliofanyika Mbala Kijiweni, kitongoji cha Mbala kwenye kijiji cha Chamakweza kata ya Pera .

 Meneja wa Kampeni za Ubunge CCM Jimbo la Chalinze Ndugu Steven Kazidi akizungumza na viongozi wa wafugaji wa kijiji cha  Chamakweza kata ya Pera wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Mbala Kijiweni.
 Mgombea Ubunge wa CCM Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wafugaji wa kijiji cha Chamakweza ,Ridhiwani alihutubia wafugaji hao ambao walimueleza kuwa wanatatizo kubwa la majosho ya mifugo yao na wanaamini yeye akiwa Mbunge atawasaidia katika kuboresha miundo mbinu itakayowasaidia kufuga kwa kisasa zaidi.
Wananchi wa Bwawani Pingo wakielekea kwenye uzinduzi wa Shina la Wakereketwa la CCM lililokuwa likizinduliwa na mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.

MWANAMKE BORA WA MWAKA 2014

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda kesho atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013-14, itakayowakutanisha wanawake wanne itakayofanyika leo katika Ukumbi wa The African Dream mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndiye atakuwa mgeni rasmi katika utoaji tuzo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, ambayo ndiyo iliyoratibu zoezi hilo, Eric Shigongo, alisema jana kwamba shughuli hiyo itakuwa ni hitimisho la kazi kubwa ya kupokea na kuchuja kura zilizotumwa na wasomaji kumtafuta mwanamke bora ambaye ni nembo kwa taifa.
Prof. Anna Tibaijuka.

“Zoezi hili lilifanyika kwa muda wa miezi tisa, kuanzia Juni mwaka jana hadi Machi mwaka huu. Awali kabisa watu walitakiwa kutuma majina ya wanawake wanaowaona ni bora ili wapigiwe kura, watu waliitikia vizuri sana, kwani jumla ya majina 150 yalitumwa katika kipindi cha miezi miwili.
Dk. Asha Rose Migiro.

“Baada ya hapo majina hayo yakaandikwa katika magazeti na watu wakatakiwa kupiga kura ili kuwatoa wanawake ambao wanadhani hawakustahili tuzo hizo,” alisema Shigongo, ambaye kampuni yake inatoa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi na Championi.

Alisema katika awamu ya kwanza ya miezi hiyo miwili, majina ya wanawake 20 yaling’ara na hivyo kuingia katika awamu nyingine ya kupigiwa kura, ambapo baada ya muda kama huo pia, wanawake kumi walipata alama nyingi na hivyo kuingia katika awamu ya tatu na ya mwisho.
Mh. Anne Kilango Malechela.

Alisema kwenye hatua hiyo ya mwisho, wanawake watano walipita ambao ni Ananilea Nkya, Anna Tibaijuka, Anna Kilango Malecela, Asha Rose Migiro na mama Maria Kham. Katika zoezi hilo, wanawake hao wenye mvuto katika jamii walichuana na mmoja wao, Nkya, kuondolewa baada ya kura zake kutotosha kwa ajili ya fainali,” alisema Shigongo.
Dk. Maria Kamm.

Kwa upande wake, mratibu wa Tuzo hizo, Luqman Maloto, alisema tukio hilo la kihistoria ambalo pia litashuhudiwa na wabunge wa Bunge la Katiba walio mjini Dodoma, litaambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali, akiwemo Linah,” alisema Maloto.

RAIS KIKWETE APOKEA RIPOTI YA MAHESABU YA SERIKALI IKULU JIJINI DAR

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Ripoti ya mwaka ya Hesabu za Serikali kutoka kwa  Mthibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh  Ikulu jijini Dar es salaam Machi 28.2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza muhtasari toka kwa  Mthibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh kabla  ya kupokea Ripoti ya mwaka Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

Airtel yaipongezwa Serikali kwa kuchangia maendeleo ya elimu

Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brighton Majwala akimkabidhi vitabu vya sayansi kwa mkuu wa wilaya Arusha John Mongela kwa ajili ya shule ya sekondari Naura ya jijini Arusha vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya airtel chini ya mpango wake wa Shule Yetu.
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela akimkabidhi vitabu mbalimbali mkuu wa shule ya sekondari Naura Sunday Mushobozi vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania katika hafla iliyofanyika shuleni hapo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari naura ya jijini Arusha wakiangalia vitabu mara baada ya kukabidhiwa vitabu hivyo na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.

RADIO 5 YAKULETEA BACK COLLEGE BASH NDANI YA NEW LANDMARK RESORT JUMAMOSI HII


MAELFU WAJITOKEZA KUUGA MWILI WA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA MARA MAREHEMU JOHN GABRIEL TUPA


 MWILI WA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA MARA JOHN GABRIEL TUPA UKITOLEWA KWENYE NDANI YA MAKAZI YAKE


 WAOMBOLEZAJI WAKIWA NYUMBANI KWA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA


 KUTOKA KUSHOTO KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MARA POUL KASABAGO,M NEC WA CCM CHRISTOPHER GACHUMA,M NEC WA BUNDA CCM...
 KUTOKA KUSHOTO MWAKILISHI WA CHANEL TEN AUGUSTINE MGENDI,GEORGE MARATU WA ITV NA FLORENCE FOCAS WA MWANANCHI
 MWENYEKITI WA BAKWATA MUSOMA MJINI AKIWA NA ASKOFU MSONGANZILA WA KANISA KATORIKI
 RAIS WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA KENETH SIMBEYA AKITOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI
 MTOTO WA MAREHEMU AITWAYE GABRIEL JOHN TUPA AKITOA SHUKURANI
 MJANE WA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE ALIKUWA MMOJA WA WAOMBOLEZAJI
 ASKOFU MSONGANZILA AKIWEKA SAHIHI KWENYE KITABU CHA WAOMBOLEZAJI
 AKIAGA MWILI
 MMOJA WA WAANDISHI WA HABARI NGULI BIGAMBO JEJE AKIAGA MWILI
 SEHEMU YA WAOMBOLEZAJI WAKIENDA KUAGA MWILI

 MKURUGENZI WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA ABUBAKAR KARSAN MWENYE MIWANI HUKU NYUMA YAKE NI MADARAKA NYERERE NAO WAKIAGA MWILI

 MGENDI WA CHANEL TEN AKIWAJIBIKA KUWAPA WATANZANIA TAARIFA
 WANAFUNZI WA SHULE PIA WALIHUDHULIA
 NAMI NILIMUAGA MKUU WA MKOA JOHN TUPA,KWA KWELI NI PIGO
 ASKARI KARIM AKIWA KWENYE GARI LILILOBEBA MWILI WA MAREHEMU
 MWILI WA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA MARA LIKIWA KWENYE GARI MAALUMU UKITOKA KWENYE MAKAZI YAKE KWENDA KANISANI
 MWILI UMEPOKELEWA LANGO KUU LA KANISA KATORIKI
 MKE WA JOHN TUPA WA PILI KUTOKA KUSHOTO AKIWA NA WANAFAMILIA KANISANI
MAELFU ya wananchi wa mkoa wa Mara pamoja na mikoa jirani wakiongozwa na viongozi wa Serikali,Dini na vyama vya Siasa wameuaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa aliyefariki juzi asubuhi akiwa wilayaniTarime kwa shughuli za kikazi.

Akitoa salamu za rambirambi za Serikali mkoani Mara,Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Bartazal Kichinda alisema walipokea kwa masikitiko makubwa msiba wa ghafla wa mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa  kwa kuwa msiba huo umekuja wakati mchango  na usaidizi wa kiongozi huyo ukiwa unahitajika zaidi mkoani Mara.
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA SHOMARI BINDA

March 27, 2014

WAJERUMANI KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UJANGILI

DSC_0080
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Frank Steinmeier akizungumza waandishi wa habari kwenye mkutano huo jijini Dar es Salaam na kuelezea mafanikio ya ushirikiano wa nchi hizo mbili. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe.(Picha na Zainul Mzige).

Na Damas Makangale, MOblog

HUKU Tembo wakiendelea kuuawa katika mbuga kadhaa nchini, Serikali ya Ujerumani imeahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kupambana tatizo la ujangili Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe amesema serikali ya ujerumani imeahidi kutoa msaada wa vifaa na ujuzi wa kupambana na ujangili katik mbuga za Tanzania.

“tupo katika hatua za mwisho za ushirikiano wa kupambana ujangili na majangili ili kunusuru Tembo wetu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo,” amesema Membe.

Waziri Membe amesema kwamba serikali ya Ujerumani imetoa magari ya kupambana ujangili, camera, vifaa vya kisasa na mafunzo kwa askari wa wanyamapori ili kuwajengea uwezo wa kupambana na majangili nchini.
DSC_0048
Picha juu na chini ni Baadhi ya wageni waalikwa na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Ujerumani nchini.

Amesema tatizo la ujangili si la Tanzania peke yake linahitaji ushirikiano na nchi mbalimbali za Afrika na ulaya kwa sababu pembe za ndovu kuuzwa kwenye nchi hizo au kuwa kama njia ya kupitishia.

“wanatoa mafunzo ya kutosha kwa askari wetu wa wanyamapori ili waweze kukabiliana kikamilifu na majangili,” aliongeza

Waziri Membe alizungumza kwenye mkutano wa pamoja na Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Ujerumani Dkt Frank-Walter Steinmeier ambaye alitembelea nchini kwa mara ya kwanza tangu kushika nyadhifa hiyo

Kwa taarifa ambazo zipo ni kwamba Tembo 25,000 waliuawa mwaka 2011 na 22,000 waliuawa mwaka 2012, ni ishara inayoonyesha kuwa biashara haramu ya wanyama pori sasa imekuwa ni uhalifu wa kidunia wenye nguvu ya kuathiri maendeleo ya kiuchumi, kusababisha migogoro, kuimarisha vikundi vya kigaidi na kuathiri watu wenye hali duni ya watu waishio katika umaskini.
Faru wanauawa na maharamia kila baada ya dakika 10 na ni wachache kuliko chui 3,500 ambao wamebaki porini.

Ujangili unaathiri jamii barani Afrika, hususan yale maeneo katika bara ambapo wanakabiliwa na hali mbaya ya janga la ujangili.
DSC_0054
DSC_0045
Sehemu ya waandishi wa habari nchini pamoja na waandishi kutoka nje ya nchi waliohudhuria mkutano huo jijini Dar.