Tangazo

April 23, 2014

Washiriki wa kliniki ya Airtel Rising Stars kutoka nchini Sierra Leone wawasili nchini

Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius mara ya kupokea timu ya Airtel Rising Stars kutoka Sierra Leone ambao watahudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mchezaji Fatmata Mansaray wa timu ya Airtel Rising Stars chini ya miaka 17 kutoka Sierra Leone, akiongea na waandishi wa habari baada ya kufika Dar es Salaam kuhudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Wachezaji wa Airel Rising Stars kutoka Sierra Leone wakiwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXx

Wachezaji sita na kiongozi mmoja kutoka Sierra Leone waliwasili jijini Dar es Salaam jana asubuhi tayari kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa ya siku tano itakayofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia kesho, Jumatano 23 Aprili, 2014. Washiriki kutoka Madagascar walitajiwa kutua jijini jana usiku.

Kwa mujibu wa kuwasili kwa wachezaji, wengi wao wanatarajia kufika leo mchana na baadaye usiku kuhudhuria mafunzo hayo yanayoshirikisha zaidi ya wachezaji 72 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Seychelles na mwenyeji – Tanzania.

Wachezaji hao chipukizi, wasichana na wavulana, walijipatia tiketi ya kushiriki kliniki baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars kwenye nchi zao pamoja na timu zilizotwaa uchampioni wa mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini Nigeria mwaka jana.

Kliniki hii itaendeshwa na wakufunzi kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United ikiwa na lengo la kutoa mafunzo ya kuwawezesha wachezaji na kuwajengea uwezo wa kutandaza kabumbu ya kusisimua hasa katika idara ya ushambuliaji.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi inayotarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka wizara inayohusika na michezo, shirikisho la mpira wa miguu nchini, Airtel Tanzania na wadau wengine wa soka.

Hii ni fursa nyingine muhimu kwa wachezaji hao chipukizi chini ya umri wa miaka 17 kuonyesha vipaji vyao na kujiendeleza kisoka. 

Program ya Airtel Rising Stars ni mpango wa maendeleo ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 barani Afrika ukidhaminiwa na kampuni ya simu za kiganjaji ya Airtel na kuungwa mkono na Manchester United. Lengo lake ni kusaidia kuibua vipaji vya soka kutoka ngazi ya chini (grassroots) hadi Taifa.

No comments: