Kaimu Mkurugenzi wa
Huduma za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila akifungua mkutano wa tatu wa wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares
Salaam.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Serikali inaandaa mpango
wa kutoa huduma za magonjwa yasiyopewa kipaumbele(NTD,s) kwa pamoja ili kuweza
kufikia watu wengi kwa kupunguza gharama.
Hayo yamasemwa leo na
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Dk,Neema Rusibamayila wakati akifungua mkutano wa tatu wa wa siku
tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo unaoendelea kwenye
hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
“ Tumekutana na wadau
mbalimbali katika mkutano huu lengo ni tunataka kuandaa mpango wa kutoa
huduma na dawa kwa magonjwa yasiyopewa kiupaumbele kwa pamoja badala ya
ugonjwa mmoja pekee.Tunaweza kupata matokeo zaidi na kusaidia kuwafikia
watu wengi kwa kuwa utarahisisha utendaji kazi, utoaji elimu na dawa,”
alisema Dk. Neema.
Dk. Neema aliyataja
magonjwa hayo kuwa ni Usubi, Trakoma, Kichocho, Minyoo, Mabusha na Matende.
Aliongeza kuwa hivi
sasa huduma hiyo imeweza kufikia wilaya 108 kati ya 160.Hivyo
changamoto iliyopo ni kufikia mikoa saba.
Alisema mpango huo
ulianza mwaka 2012 na unaendelea hadi mwaka 2017, ambapo mafanikio yameonekana
mfano katika kupambana na ugonjwa wa usubi utafiti ulifanyika umeonesha
kuwa kati ya wilaya tisa ni wilaya mbili ndizo zitaendelea kupatiwa dawa.
Naye Meneja Mpango
wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele(NTD,s),Dk, Upendo Mwingira alisema
changamoto nyingine iliyopo katika kubabiliana na magonjwa hayo ni baadhi ya
jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya magonjwa hayo ambayo dalili zake si rahisi
kuonekana kwa macho kwani huonekana baada ya muda mrefu mfano Matende na
Mabusha.
Alisema baadhi ya
jamii huwa mwitiko mdogo wakati wa utoaji wa huduma, hivyo
Dk. Upendo aliitaka jamii kujitokeza kwa wingi wakati wa utoaji wa huduma hizo.
Alizitaja baadhi
ya athari ya magonjwa hayo kuwa ni ulemavu wa kudumu na miongoni mwa sababu
zinazochangia kuwepo kwa matataizo hayo ni umasikini.
No comments:
Post a Comment