Tangazo

November 30, 2017

WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG


 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akifafanua baadhi ya mambo wakati viongozi wa Mfuko walipokuwa wakiwasilisha taarifa za utendaji wake kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC, jijini Arusha leo Novemba 30, 2017.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) umepata hati safi katika taarifa ya hesabu zake za fedha katika kipinmdi cha mwaka 2015-2016 ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.

Katika taarifa hiyo mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2016 (mwaka wa kwanza tangu kuaza kufanya kazi zake), thamani ya Mfuko ilifikia shilingi bilioni 65.68 na mfanikio haya yaliweza kufikiwa kutokana na ubunifu na ushirikiano mkubwa kati ya Mtendaji Mkuu wa Mfuko na Bodi ya Udhamini, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Mfuko huo, Bw.Bezil Kwala, aliwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa Mfuko huo unaoingia siku yake ya pili nay a mwisho kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha, wakati akiwasilisha taarifa hiyo ya fedha leo Novemba 30, 2017.
Amesema Mfuko umekuwa ukiaandaa hesabu zake kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uaandaji wa hesabu za fedha na kwa mujibu wa sheria CAG ndiye mwenye mamlaka ya kufanya ukaguzi na Hati Safi ni uthibitisho wa taarifa ya fedha za Mfuko kuonyesha hali halisi na kutokuwa na dosari ya aina yoyote.
Amesema katika ukaguzi huo, CAG alishirikiana na kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC). Mwakilishi wa kutoka Ofisi ya CAG, Bw…….. amethibitishia wajumbe usahihi wa taarifa hiyo ya fedha ya WCF.
Mkutanmo huo ambao umeanza Novemba 29, 2017 na kubeba kauli mbiu isemayo, "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”, pia ulipokea taarifa ya mipango ya uwekezaji ambapo Bw. Kwala aliwaambia wajumbe kuwa, katika kipindi kati ya mwaka 2017/18 – 2021/22, Mfuko umepanga kuwekeza kwenye miradi mbalimbali itakayoleta faida kwa mujibu wa tathmimi za kitaalamu zitakazofanyika.
“Maeneo tuliyoyaanisha katika uwekezaji kwenye sekta ya viwanda ni pamoja na kiwanda cha Grape Processing Factory kwa ushirikiano kati ya  GEPF na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, kiwanda cha Madawa mkoani Simiyu kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Kiwanda cha Morogoro Canvas Mills kwa kushirikiana na mifuko ya WCF, NSSF, PSPF, GEPF, na LAPF”. Alifafanua.
Akifafanua zaidi kuhusu umuhimu wa Mfuko kuwekeza, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba alisema, fedha zitokanazo na michango ya Wanachama ni kidogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya ulipaji Mafao ya fidia na kwa hali hiyo, ni muhimu Mfuko kuwekeza ili kupanua wigo wa kuongeza mapato na hivyo kuendelea kutoa Mafao ya Fidia bila ya shaka yoyote.

 Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa WCF wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, akizungumza
 Mkurugenzi wa Fedha WA WCF, Bw.Bezil Kwala, akiwasilisha ripoti ya fedha ya Mfuko kwa mwaka wa 2015-2016.
 Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Ofisi ya Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Johanes Joel Kisiri, akisikiliza uwasilishaji wa taarifa hiyo ya fedha.
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria cha WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu Sheria juu ya kuanzishwa kwa Mfuko na jinsi unavyofanya kazi zake. Pamoja na mambo mengine Bw. Siyovelwa aliwaambia wajumbe kuwa,   Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoazishwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura Na. 263 (Marejeo ya 2015) na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Julai 2015. Lengo la kuazishwa kwa Mfuko ni kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi waliopo katika sekta rasmi (Binafsi na Umma) Tanzania bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anslem Peter, akiwasilisha taarifa ya uendeshaji ya Mfuko katika kipindi cha uahai wake, ambapo alisema Mfuko umekuwa ukifanya vizuri ikiwa ni pamoja na usajili wa wanachama " katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015-2017 jumla ya Waajiri 5,178 walisajiliwa ikiwa ni asilimia 71.92 ya lengo la kusajili waajiri 7,200

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Dkt.Irene Isaka.
 Kiongozi wa chama cha Waajiri nchini (ATE), Bw. Aggrey Mlimuka, akizungumza kwenye mkutano huo.
 Bw. Hiroshi Yamabana kutoka Shirika mla Kazi Duniani, (ILO), akiuliza masuala mbalimbali kuhusu upembuzi juu ya usalama mahala pa kazi
 Tommie Dounball, kutoka kampuni ya Argen ya Afrika Kusini, akizungumzia uzoefu wa masuala ya Mfuko wa Fidia kutoka nchini kwake

 Bw. Mshomba (kushoto), akizungumza jambo wakati wa mkutano huo. Kulia ni Bw.Tommie Dounball, kutoka kampuni ya Argen ya Afrika Kusini,

 Mbunge wa jimbo la Mlalo Mkoani Tanga, Mhe. Rashiud Shangazi, (kushoto), akimsikiliza Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele. Wote hao ni miongoni mwa wadau walioalikwa kushiriki mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wdhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, (kulia), akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Taifa wa Bima ya Afya, (MHIF), Bw. Afya, Bw. Bernard Konga.
Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Lightness Mauki

No comments: